THE AFRICAN
BEAUTY IN THE DARKNESS
(UZURI WA
AFRIKA ULIOFICHWA/ GIZANI)
Kabla ya
kuja wakoloni waafrika tulikuwa na utamaduni wetuwenyewe, utamaduni ambao
tuliuona kama ni utukufu kwetu, tulikuwa na dini yetu wenyewe kwa kuabudu miungu mblimbali kama mawe, miti,
wanyama na miamba.Tulikuwa na jinsui ya uvaaji wetu wenyewe ambapotulikuwa
tukivaa ngozi za wanyamana masalia ya mimea pia, lakini baadaye kidogo
tulivamiwa na wageniambao walikujana utamaduni wao mpya na kutakasisituufuate,
waliuchukia utamaduni wetu na kuuita ni utamaduni wa kishenzi yaani usio na maana wala manufaa, taaratibu
tukaanza kuwafuata na kuwaamini, leo hii Afrika yetu imetawaliwa na umagharibi
kwa kiasi kimkkubwa na tunaona mambo mengi yanayoendelea sasa kutokana na
autamaduni huu.
Lakini cha kujiuliza hivi ni kweli
kwamba utamaduni wetu wa muafrika
unakasoro? Sawa zinaweza kuwepo lakini hatuwezi
kusema utamaduni wetu haufai!! Kikubwa nilichojifunza ni kwamba
utamaduni wa muafrika ni utamaduni wa kipekee na unafaa kuigwa kwani
kuna mambo mazuri ndani yake lakini
sasa utamaduni wa magharibi ambao ndio giza lenyewe unajitahidi mno kufunika utamaduni wetu ili usionekane
kabisa.Kutokana na hali hiyo basi ndio
nikapata sentensi hii “UZURI WA AFRIKA GIZANI” Kwamba licha ya kufunikwa bado tunajitahidi
kuionyesha dunia kuwa tuna mengi ya kujivunia kama waafrika.
HAMASISHO
•
Mitindo hii nimeifanya kutokana na ukweli wa maisha waliyoishi babu
zetu kabla ya ukoloni.
•
Pia nimefanya kwa kuangalia historia ya mapigano/vita vya wakati huo.
•
Aidha nimehamasishwa sana na ule utawala wa zamani wa Mfalme na
malkia.
VIFAA
Nguo hizi
zitatengenezwa kwa kutumiavifaa mbalimbali ambavyo ni vya kiasili mno kama
mimea na masalia ya wanyama, kwa hiyo tutaona ngozi za wanyama, vifuu vya nazi
, na mabati , ukindu , mikeka na
magunio.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)