
Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha.



Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha.


Katika kuhakikisha madereva wanaosambaza bidhaa za kampuni wanafanya kazi zao kwa ufanisi,kampuni ya TBL Group imeandaa mafunzo maalumu kwa madereva kutoka viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Moshi,Mbeya na Mwanza.
Mafunzo hao ambayo yamemalizikia mkoani Arusha yaliendeshwa na mkufunzi wa madereva kutoka kampuni ya CFAO Motors,Hubert Kubo ambaye amewapatia madereva hao elimu ya udereva wa kujihami ikiwemo utunzaji wa vifaa wanavyoviendesha.
Baadhi ya madereva waliohudhuria mafunzo hayo walishukuru mwajiri wao kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali kuhusiana na kazi yao ambayo walidai yanawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi na kuwa na uwezo wa kukabili changamoto mbalimbali za kikazi kwa urahisi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)