EAGT watoa msaada jijini Mwanza - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

EAGT watoa msaada jijini Mwanza

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG

Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.


Akikabidhi msaada huo hii leo, Askofu wa kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola, amesema watoto 18  waliokabidhiwa msaada huo ni sehemu ya watoto 264 wanaolelewa na kanisa hilo kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto iliyoanzishwa kanisani hapo tangu mwaka 2010.


Askofu Dkt.Kulola amesema hiyo si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa msaada wa vitu hivyo na kueleza kuwa limekuwa likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.


Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel, amesema msaada huo umetolewa baada ya uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.


Wazazi, walezi na watoto walionufanika na msaada huo, wameushukuru uongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.


Msaada huo wa vitanda, magodoro, mashuka, mahindi na mchele umegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa ambazo zilitolewa na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo cha Huduma ya Mtoto ambacho kiko chini ya Kanisa hilo.
Mmoja wa watoto walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya watoto wengine
Mmoja wa wazazi/walezi walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya wazazi/walezi wengine
Mmoja wa wazazi/walezi walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya wazazi/walezi wengine
Watoto baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
Watoto baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
Mtoto katika ubora wake
Msaada wa vyakula kwa watoto wanaolelewa na Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Kila mmoja katika jamii anao wajibu wa kuhakikisha mtoto anapata malezi bora

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages