Pages

Copa America Centenario 2016. Wenyeji waanza kwa kichapo

Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

Hatimaye utepe wa mtanange wa michuano ya Copa Amerika umekatwa alfajiri ya kuamkia leo, mishale ya saa 10:30 kwa saa za hapa nyumbani na kushuhudia wenyeji wa michuano hiyo, Marekani wakianza vibaya kwa kuchabangwa mabao 2-0 na watukutu wa Colombia.

Mchezo ulianza kwa kasi na kumilikiwa zaidi na Colombia ambao iliwachukuwa dakika 8 tu kujipatia goli la kwanza, goli lililotokana na uzembe wa walinzi wa Marekani kushindwa kuokoa mpira wa kona iliyochongwa na Edwin Cardona's na kumkuta Christian Zapata na kuuweka kambani mpira huo.

Wenyeji walijitahidi kufurukuta ili kusawazisha bao na kunako dakika ya 36 Clint Dempsey mchezaji aliye wasumbua sana Colombia alikosa bao baada ya shuti lake kuokolewa na golikipa Aspira, mpira huo ulisababisha Colombia kufanya shambulizi la kushitukiza (counter attack) na katika harakati za kuokoa mlinzi wa Marekani Yedlin akaunawa mpira na mwamuzi Roberto Gacia toka Mexico akaamuru upigwe mkwaju wa penati.
Wachezaji wa Marekani pamoja na kocha wao Jurgen Krinsman walijaribu kugomea penati hiyo kwa kumzonga mwamuzi lakini haikusaidia kitu maana refa ndiyo mwamuzi wa mwisho, unajua akisema nyinyi ni nyani basi ni nyani, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez akaukwamisha mpira kimiani kiufundi kabisa na kufanya ubao usomeke 2-0.

Kipindi cha pili Marekani walijitahidi angalau kupata hata goli la kufutia chozi lakini bahati haikuwa yao maana kunako dakika ya 58 Clint Dempsey aliyekuwa akilitia njaa goli la Colombia alipiga kichwa mpira wa kona na kumpita kipa Aspina lakini mpira huo uliokolewa kwenye mstari na mlinzi Perez na kunako dakika ya 64 Clint Dempsey alipiga free kick matata sana iliyookolewa na golikipa Aspina, hivyo kipyenga cha mwisho kilipopulizwa COLOMBIA 2 MAREKANI 0.

Patashika hiyo itaendelea leo kwa michezo mitatu

COSTA RICA vs PARAGUAY
BRAZIL vs EQUADOR
HAIT vs PERU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)