Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania,DK.Gift Shoko akiongea na wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) waliohudhuria futari maalumu iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Imam Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa akitoa mawaidha wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya CBA katika Hoteli ya Serana jijini Dar es Salaam, jana kwa ajili ya wateja wakati wa kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA,Dk.Gift Shoko (wa nne kushoto ) na Imam Mkuu wa Masjid Ma,Amour Sheikh Issa Othuman Issa (wa tano) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.
Baadhi ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Benki ya
CBA Tanzania imewafuturisha baadhi ya wateja
wake wa jijini Dar es Salaam ikiwanisehemuyakuboreshauhusianonawatejaambapo pia itawaandaliawateja wake futarikwenyemaeneombalimbali yalipomatawinchini
.
Akizungumzawakatiwafutariiliyoandaliwana
CBA Tanzania kwa wateja katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk.Gift
Shoko alisema “
Tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili
pia
tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii”.
Alisema Benki ya
CBA Tanzania huwa inakutana na kushirikiana na wateja wake
katika masuala mbalimbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika matukio ya kuchangia kuinua sekta mbalimbali mfano afya na elimu.
“Lakini leo ni siku muhimu kwetu hapa Dar es Salaam
kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani ambao unaendelea”.
Dk.Shoko aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma za keili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na kubuni huduma mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji kupata huduma za kibenki na kuboresha shughuli zao.“Benki ya
CBA Tanzania tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia
maandalizi mema ya sikukuu!, endeleeni kufurahia huduma zetu mbalimbali na msiache kutembelea matawi yetu au
kutembelea mtandao wetu kwa njia ya kisasa ya kuona huduma zetu mbalimbali kama
vile huduma ya mkopo wa bima ambayo inaonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi,mikopo ya kununua nyumba yenye masharti nafuu
pia tunatoa huduma ya M-Pawa kwa kushirikiana na Vodacom inayowezesha wateja wa
M-Pesa kuweka akiba na kupata mikopo kwa haraka na bila masharti magumu.” Alisema
Benkiya
CBA Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo. Bado
CBA ina mpango wa kutoa misaada katika mikoa mbalimbali kwa dhumuni la
kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.
CBA
Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania,
CBA Tanzania ina matawi kumi na moja yaliyosambaa sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)