Airtel yafuturu na Bloggers - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Airtel yafuturu na Bloggers

Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel.
Mlimiliki wa 8020 blog Shamimu akiuliza swali mara baada ya kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye mkutano ulifatiwa na Futari
Baadhi ya Bloggers wakijaribu kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu zao na ipad zao
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa kwenye Futari baada ya mkutano wa VSOMO
Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na Shamimu mmiliki wa blog ya 8020 na  Josephat Lukaza mmiliki wa lukaza blog,  wakati wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO, mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel.
Baadhi ya bloggers wakipata futari
Katika mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani leo Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana na bloggers na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo VSOMO, mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya Airtel.

Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya alisema, ana matumaini kuwa masomo ya Ufundi yanayotolewa kupitia VSOMO kwa kushirikiana na VETA kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kutobahatisha na kuongeza ufanisi katika kazi zao.

Nao bloggers waliohudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu. Aidha waliongeza kwa kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages