UINGEREZA YAIFAGILIA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, JKCI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UINGEREZA YAIFAGILIA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, JKCI

 Kaimu Muuguzi Mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Flora Kasembe, (wapili kulia), akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi cha JKCI, wakati Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (wapili kushoto), alipotembelea kambi ya upasuaji wa moyo iliyoendeshwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya hiari ya Uinegereza ya Muntada Aid, Mei 3, 2016. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Mohammed Y.Janabi, Meneja Mradi wa Muntada Aid, Kabir Miah, Mkuu wa Upasuaji wa JKCI, Dkt.Peter Kisenge, na Daktari Bingwa wa Moyo wa JKCI, Dkt.Tulizo Shem

Profesa Janabi (kushoto) na Balozi Sutherland baada ya kutembelea chumba cha Coronary care unit
NA K-VIE MEDIA/Khalfan Said
NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (pichani wapili kushoto), ameisifu taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa. Pongezi hizo amezitoa leo May 3, 2016, baada ya kutembelea kambi hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo, na kujionea madaktari wakiendelea na kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini.

“Nimefurahishwa sana na uamuzi wa JKCI wa kuratibu zoezi hili kwa ushirikiano na wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nje ya nchi, najua
taasisi ya hiari kutoka Uingereza imekusanya fedha na kwa kushirikiana na
madaktari wengine, wamewezesha zoezi hili kufanyika kwa mafanikio.” Alisema Balozi Sutherland.

Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake
nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, na hatimaye kwa kushirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI wameweza kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Janabi alisema, chini ya uratibu wa taasisi yake, wataalamu kutoka Australia kupitia Open Heart
International, wakishirikiana na wataalamu kutoka JKCI waliendesha kambi  ya upasuaji wa moyo kwa watoto 15 kuanzia
Aprili 25 hadi Aprili 30.

“Kambi hii ya sasa, inaundwa na wataalamu kutoka Saudi Arabia
chini ya uratibu wa taasisi ya hiari ya Muntada Aid, yenye makazi yake nchini Uingereza, na hadi leo hii Mei 3, 2016, tayari watoto 20 wameshafanyiwa upasuaji na hivyo kufanya jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji tangu kambi hizi mbili zianze.” Alifafanua Profesa Janabi kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Profesa Janabi alisema, malengo yao ni kuwafanyia upasuaji watoto 70 Ifikapo Mei 7. “Tunawashukuru wenzetu hawa kwa kuja kutshirikiana
nasi kwani upasuaji unaofanyika ni huu wa kisasa, ambapo hakuna kumpasua kifua mgonjwa bali tunafanya upasuaji kwa kutumia matundu na hili ni jambo muhimu kwa wataalamu wetu ambao wamepata fursa ya kujifunza kutoka kwao.” Alisema.
 Profesa Janabi (wapili kulia), wengine kutoka kulia, ni Balozi Sutherland, Dkt. Shem, na Dkt.Delila Kimambo
 Wataalamu wa JKCI wakiwa kazini kwenye mojaya vyumba vya upasuaji
 Balozi Sutherland, katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka JKCI na wale wa Muntada Aid
 Profesa Janabi, akimsikiliza mgeni wake, Balozi Sutherland
 Dkt.StellaMongella. (kushoto, akimpatia maelezo Balozi Sutherland, alipotembelea wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji (Post Operative Recovery Word), Kulia ni Profesa Janabi
 Balozi Sutherland, akiwapongeza wataalamu wa moyo kutoka Muntada Aid, wanaoshuhudia ni Profesa Janabi (kulia na Dkt. Tulizo Shem kutoka JKCI.
 Baadhi ya Watanzania wakisubiri huduma ya matibabu ya moyo
 Kiongozi wa timu ya madaktari kutoka Muntada Aid, (katikati)
 Dkt. Tulizo Shem akiongea
Balozi Sutherland akipokewa kwenye taasisi alipowasili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages