Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK (kushoto) akisoma taarifa ya Snura Mushi kuomba msamaha kwa Watanzaniaya kutokana na kusambazwa kwa video ya msanii huyo iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi (kulia) akiomba msamaha mbele ya Watanzania kutokana na kusambaza video yake iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
NA KHADIJA KALILI
Ikiwa ni siku moja tu tangu Wizara ya Habari , Utamaduni Sanaa na Michezo jana kutangaza kumfungia msanii Snura Mushi kujihusisha na masuala ya sanaa ikiwemo kutumbuiza kutokana nawimbo wake wa Chura ambao aliusambaza kwenye mitandao ya kijamii You tube, WhatsApp na mingine mingi kutokana na kurekodiwa kinyume na maadili ya Mtanzania.
Ndipo leo asubuhi Snura alipoibukia kwenye Ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari MAELEZO,Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na vyombo mbalimbali vya habari.
Baada ya kuwasili ukumbini na kutambulishwa Snura alianza kwa kusema "Karibuni ndugu zangu waandishi wa habari , naitwa Snura Anthony Mushi wengi wananifahamu kwa jina la kisanii Snura, na kulia kwangu ni msimamizi wa kazi zangu za sanaa 'Meneja' wangu Hemed Kavu almaarufu kwa jina la HK.
Kwanza tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa kuitikia wito huu:
"Tumewaita hapa leo kwa ajili ya kuomba radhi umma wawatanzania kwa ujumla kwa kosa l;a kutengeneza , kuzindua na kuweka mtandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke isiyozingatia maadili ya kitanzania ya muziki unaoitwa 'Chura' alisema Snura.
"Tunaviomba radhi vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutofuata sheria , kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa nchini".
"Mimi na Meneja wangu tunaahidi kutorudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji , na iwapo tutarudia basi tupewe adhabu kali kwa mujibu wa sheria za nchi hii" alisema Snura.
Aliendelea kwa kusema kuwa "pia tunaahidi kuwa mfano bora kwa jamii inayowazunguka na kwa wasanii hususan katika masuala yahusuyo kutunza na kufuata maadili na utamaduni wetu pamoja na sheria za nchi. Hii ni pamoja na kupata vibali katika mamlaka na taasisi zinazohusika".
Katika hali isiyokuwa ya kawaida pia Snura amekiri kuwa alikua akifanya shughuli zake za sanaa bila ya kuwa na usajili Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
"Tunafahamu kwamba baadhi ya wasanii hususan wa muziki wa kizazi kipya hawajajisajili BASATA kama ilivyokuwa kwangu mimi lakini kwa sasa baada ya kupata maelekezo kutoka (BASATA), nimeshapata usajili na sasa natambulika kisheria.
Snura aliweka wazi kuwa yeye binafsi aliitwa Wizarani na kuhojiwa kuhusu wimbo wake wa Chura hivyo alitambua kwamba utafungiwa akagundulika hakuwa na usajili BASATA.
Alisema sharti la kwanza alilopewa ilikuwa ni kuitoa video ya Chura kwenye mitandao ya kijamii You Tube kutokana na namna ilivyorekodiwa." Tayari hili limeshatekelezwa na video imeshafutwa kwenye akaunti hiyo. alisema HK.
Pia tayari Snura ameshasajiliwa BASATA hivyo yuko huru kufanya kazi katika maonyesho yake ya sanaa .
Akizungumzia kuhusu sharti la tatu ni kuiirekodi upya video na muziki ya Chura.
KWANINI CHURA IMEMDHALILISHA SNURA?
Kwa mujibu wa Snura anakiri ni kutokana na kiwango kidogo cha elimu alicho nacho pia upeo wake wa kufikiria ndiyo ulifikia ukomo hivyo asamehewe.
"Mimi sikuwa na lengo la kuwadhalilisha wanawake wenzangu kukatika viuno hapa kwetu ni jadi na mimi mwenyewe nacheza , kuhusu nguo kulowekwa maji alisema kuwa wale walivaa mitandio na walilowa maji huku akisisitiza kuwa waliona mazingira ya maisha ya Chura ni kwenye maji hivyo wao waliona sawa kujitumbukiza kwenye maji.
"Lakini jiliporudi nyumbani na kuiangalia vizuri video ya Chura nikaona ina makosa ndiyo maana sikuisambaza kwenye Luninga yoyote" alisema Snura.
Mwisho msanii huyo pamoja na Meneja wake wametoa shukrani za dhati kwa Wizara ya Habari , Utamaduni , Snaa na Michezo pamoja na BASATA kwa ku maelekezo na elimu waliyowapatia.
Juku wakiahidi kufanya kazi na kuwa mabalozi wema kama walivyoagizwa.
"Hivi sasa tunaufanyia masahihisho wimbo wa Chura pamoja na video yake na baada ya hapo utaangaliwa na Bodi ya Filamu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)