Pages

Serikali yatangaza viwango vya tozo kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere

Tayari Dar es salaam imeanza kufurahia urahisi wa kuvuka bahari kwa urahisi zaidi kwenye safari kati ya Kigamboni na Town Dar es salaam ambapo daraja lilivyozinduliwa tu tuliambiwa tutalipia ila hatukutajiwa bei, leo May 10 2016 ndio bei zimetajwa na unaweza kuzipata hapa chini.
Kaongea Injinia Joseph Nyamwuhanga kataja kila kitu >>>

‘Shughuli za kutoza fedha zitasimamiwa na shirika la NSSF na tumeweka tozo kwa watumiaji wa aina mbalimbali mfano Magari na Pikipiki na kila mmoja atalipa kulingana na aina ya chombo chake’


‘Kwa waendao kwa miguu wataendelea kupita bure mpaka Serikali itakapoweka utaratibu tofauti, wenye baiskeli tozo itakuwa shilingi 300/= ila kwa sasa watapita tu bure mpaka tutakapowatangazia siku ya kuanza kulipa, kwa wenye pikipiki watalipa shilingi 600/=, Baiskeli za miguu mitatu (Guta ) watalipa shilingi 1500/=’

‘Mikokoteni watalipa shilingi 1500/=, Pikipiki za Miguu mitatu ambazo ni Bajaji watalipa Tsh. 1500/=, Gari ndogo (Saloon Cars) watalipa kwa shilingi 1500/= Magari aina ya Pick-Up yasiyozidi tani mbili yatalipa shilingi 2000/=, ( Minibuses )


mabasi madogo yanayobeba abiria wasiozidi 15 yatalipa shilingi 3000/=, Mabasi yanayobeba abiria kati ya 15 -29 yatalipia Tsh. 5000/=, Tractor ni Tsh. 7000/=

‘Tractor yenye trailer lake hao watalipa shilingi 10,000/=, Magari yenye uzito wa tani 2 mpaka 7 watalipia 7000/=, magari yenye uzito wa tani 7 mpaka 15 watalipia 10,000/=, magari yenye uzito wa tani 15 mpaka 20 watalipia 15,000/=, magari yenye tani 20 mpaka 30 watalipia shilingi 20,000/=, Semi Trailer kama magari yanayobeba mafuta yatalipia 30,000/=, Truck Trailer watalipia shilingi 30,000/=,

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)