Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde atembelea kambi tiba ya GSM Dodoma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde atembelea kambi tiba ya GSM Dodoma

 Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI, ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya Mwanza, Singida, na Shinyanga.

Akieleza sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza, ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi kila mwaka.

"Nimeshtushwa na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo, hongereni sana", alisema Mavunde.

Mavunde amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja tu kubwa na ya msingi ya utanzania.

PICHANI JUU: Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(Wa Pili kutoka kulia) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kulia) na Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK Othman KIloloma(Wa nne kutoka kulia) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI Shannon Kiwamba(kushoto)
Mh Mavunde akisikiliza maelezo ya mmoja kati ya wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
 Mratibu wa Kambi Tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma akimpa taarifa za wagonjwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini
 Mh Mavunde akiongea na wanahabari waliokuwa hospitalini hapo kufuatilia habari za wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mh Mavunde akibadilishana mawazo na mratibu wa kambi tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma, wanaosikiliza ni Kibwana Matukio kutoka GSM, na Mganga mkuu wa mkoa Bw Jordan Rugimana

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages