Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Itifaki na Uhusianoi wa AICC, Catherine Kilinda.
Kituo cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa huo.
|
Akipokea madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni sehemu ya juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili kuhakikisha shule zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.
“Napenda niishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi Mwendeshaji Elishilia Kaaya kwa kuitikia vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Alitoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.
Akizungumza baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC kama shirika la umma linawajibu wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.
“Sisi kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto wetu wa shule hawakai chini na ndio maana leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua sekta ya elimu”, alieleza Catherine.
AICC ambayo inajihusisha na kutoa huduma za Mikutano, upangishaji w ofisi na nyumba pamoja
na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)