Bw. Huxiangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania.
Mkakati wa Huawei katika kubadili namna uonavyo dunia iliyokuzunguka Kampuni ya Huawei yaungana na Watengenezaji mashuhuri wa kamera duniani; Leica kutengeneza simu P9
Mwezi Aprili, Huawei wamezindua simu
iliyokua ikisubiriwa kwa muda mrefu katika mlolongo wao wa simu zao za P
Series; Huawei P9. Uzinduzi wa Huawei P9 umezingatia kipaumbele cha teknolojia
ya hali ya juu. Toleo hili la tisa la P Series limewezeshwa na Kampuni ya Huawei
pamoja na kampuni mashuhuri kwa utengenezaji wa camera duniani Leica. Simu hii
ina kamera ya kipekee yenye lenzi mbili, ambayo imeweka rekodi katika
teknolojia ya kamera za simu za kisasa, ikiwa na mwanga Zaidi na ubora Zaidi,
kupata picha zenye rangi nzuri Zaidi katika staili ya Leica ya kipekee.
Watanzania wanategemea kupata simu
hii yenye teknolojia ya hali ya juu na ya kipekee katika kamera hivi karibuni.
Hii inafuatia uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika mji wa Dubai wiki hii. Uzinduzi
huo wa kipekee ambao ulihudhuriwa na viongozi wa Huawei Tanzania na Waandishi
wa Habari umeashiria upatikanaji wa simu hii katika soko la Tanzania hivi
karibuni.
Tokea uzinduzi wake mji wa London,
simu hiyo imepata mapokezi makubwa kama simu “inayobadili namna uonavyo dunia”.
Simu mpya ya kipekee Huawei P9 ina malengo kubadili ubora wa picha unaopatikana
katika timu za kisasa maarufu kama “smartphone”. Teknolojia katika simu hiyo
inabadili namna tunavyopiga na kufurahia picha, hii imetokana na shauku ya
Huawei kuendelea kuvuka mipaka ya uvumbuzi, ikilinganishwa na uzoefu na kipaji
katika utengenezaji wa kamera na lenzi wa Leica pamoja na ushirikiano mzuri
katika kutengeneza P9.
Waliokuwepo katika uzinduzi huo ni
pamoja na viongozi wakuu wa Huawei Tanzania akiwemo Bwana Huziangyang Jacko,
Meneja wa Huawei nchini Tanzania, Lydia Wangari Meneja Masoko kampuni ya Huawei
Tanzania, waandishi wa Habari na wadau mbalimbali kutoka Tanzania.
Akionglea ujio wa simu hiyo katika
soko la Tanzania Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania
alisema ”Tunategemea kuleta simu mpya ya Huawei P9 kwa wateja wetu wa Tanzania
hivi karibuni; Tunaamini teknolojia hii ya hali ya juu na ya kipekee
iliyotokana na utafiti wa hali ya juu na shauku ya kubadili namna watumiaji
wetu waonavyo dunia inayo wazunguka, P9 ikifanya kazi na Leica, tumeweza
kufanya maajabu katika teknolojia ya lenzi ya kamera”.
Akiongea katika uzinduzi huo, Lydia
Wangari Meneja Masoko Huawei Tanzania alisema, ”Tunaendelea kuzindua simu mpya ,
tukitilia mkazo katika teknolojia ya kipekee. Kwa kushirikiana na wadau
wengine, tumeweza kujumuisha utamaduni, mtindo ya maisha ya wateja wetu na teknolojia
ili kuwapatia wateja watu simu bora zaidi”.
Kuongezeka kwa aina mbalimbali za
simu za mkononi za smartphone nchini Tanzania inaashiria ukuaji na umuhimu wa
Tanzania katika soko duniani huku wa Tanzania Zaidi wakigundua umuhimu wa
teknolojia maishani mwao. Mahitaji katika maendeleo na simu za kiteknolojia yanaongezeka kila kukicha nchini
Tanzania na kampuni ya Huawei imeendelea kutatua hitaji hilo nchini Tanzania.
Kufuatia mafanikio ya simu aina ya P
zijulikanalo kama “P Series”, kwa ujumla mapokezi ya simu ya Huawei P9 ni
mazuri duniani kote. Huawei Tanzania wana matarajio makubwa juu ya ufanyaji
kazi wake katika soko la Tanzania. Wakiahidi watumiaji simu yenye nguvu na
ubora wa kipekee usio linganishwa, simu mpya ya P9 itapatikana katika rangi
nne: Dhahabu, kijivu, Dhahabu iliyoiva Zaidi na Siliva huku P9 Deluxe Version
ikipatikana katika rangi ya dhahabu na Nyeupe.
Familia ya simu za Huawei P9 imetumia njia za kipekee na ubora wa hali ya
juu kubadili namna tunavyoona dunia iliyotuzunguka. Inaendeleza heshima ya
Huawei ya simu zenye ubora wa juu ambazo zimeacha alama katika soko kwa ubora
na ufanisi.
Huawei itaendelea kukamata fursa mbalimbali
ili kubadili soko na kuinuka duniani katika biashara za watumiaji wa simu za
mkononi. Huku simu za kampuni hiyo zikizidi kua na teknolojia ya hali ya juu,
Huawei itaendelea kutengeneza vifaa vinavyoweza tumika na mteja wakati wowote
na mahali popote. Na Wataendelea kuungana na wadau wengine katika soko la
vifaa, programu. Kupitia uvumbuzi wa teknolojia pamoja na kushirikiana na wadau
mbalimbali, kampuni ya Huawei ina ahidi kuleta vifaa Zaidi kwa wateja wake wote
duniani.
Kuhusu Huawei
Huawei
ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya
wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika
viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano vinatumika
katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228
ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500.
Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei
imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi
ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha
inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano duniani kote.
Kampuni
ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti
kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani.
Huawei
imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, Tigo,
Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC,
Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France
Telecom, na China Unicom.
Kupata
habari Zaidi tembelea www.huaweidevice.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)