Wauzaji kadhaa wa vifaa vya Huawei Tanzania wakitembelea Baadhi ya sehemu za maonyesho ya simu mpya za Huawei, katika mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
Baadhi ya zawadi mbalimbali zilizogawiwa kwa wauzaji wa simu za Huawei waliohudhuria mkutano mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
Timu ya Huawei Device Tanzania katika picha ya pamoja na wauzaji wa simu za Huawei nchini Tanzania waliohudhuria mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii..
Mmoja wa wauzaji wa vifaa vya Huawei akiweka sahihi katika ukuta wa wageni wa Huawei katika mkutano mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
Bw. Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania akitoa hotuba katika mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
Bw. Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania akimpatia cheti muuzaji wa simu za Huawei Tito Mahenge kuthibitisha kuwa anauza simu zilizo halisi na bora; Wakati wa mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania
Bw. Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania (kushoto) akiwapatia vyeti wauzaji wa simu za Huawei Salum Otonde na Mkewe kuthibitisha kuwa wanauza vifaa vilivyo halisi na bora, katika mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania
Huawei
yasaidia ukuaji wa wadau Tanzania.
Mkutano
wa wauzaji wa simu za Huawei Device Tanzania 2016.
Hivi karibuni Kampuni ya Huawei Device
Tanzania ilifanya mkutano wake wa kwanza wa wasambazaji wa simu za mkononi
wakitilia mkazo katika mipango ya ukuaji kwa kampuni ya Huawei Device Tanzania na
wadau wao waliopo mikoani katika soko la Tanzania kwa ujumla. Mkutano huu uliyofanyika
tarehe 30 Mwezi Aprili katika Hoteli ya Double tree jijini Dar es Salaam,
ulisherekea juhudi na msimamo wa muda mrefu wa wauzaji wa simu za mkononi Huawei
Device Tanzania.
Wauzaji waliothibitika wa simu za Huawei
nchini kote walikaribishwa. Wauzaji
waliungana na timu ya Huawei Device Tanzania kutoka mikoa yote mikuu
kama, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, Dodoma, Tanga, Morogoro,
Singida, Kagera, Kigoma na Bukoba.
Katika mkutano huo, Huawei Device
Tanzania waliweka msisitizo katika haja ya kusaidia ukuaji kwa kutoa motisha
kubwa. Bwana Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania alitangaza
kuwa 10% ya mapato ya Huawei Device Tanzania yatatengwa kama uwekezaji wa
kimasoko ili kuongeza na kuboresha bidhaa za Huawei.
Akiongea katika mkutano huo, Bwana Hu
Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania alisema “tunafuraha
kuweza kuzungumza na wadau wetu ambao watatuwezesha kuwa wauzaji wa simu za
mkononi bora na namba Moja nchini Tanzania, kutoka nafasi ya Pili ambapo tuna %
22 ya hisa katika soko” (Q1, 2016).
Pia kutoa motisha Zaidi, Huawei
walitangaza mpango mahususi ambapo wauzaji wakuu watazawadiwa dola za
kimarekani 20,000 kwa mshindi wa kwanza na nafasi ya pili atapewa dola za kimarekani
10,000.
Bwana Wang aliwapongeza Zaidi wauzaji
kwa kusaidia Huawei Device Tanzania na Zaidi ya wauzaji 50 walipewa vyeti
kuthibitisha kuwa wanauza simu halisi na orijino za Huawei.
Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa
Huawei Device nchini Tanzania pia aliwapongeza wasambazaji na wauzaji wa
rejareja waliokuwepo kwa ufanyaji kazi wao mzuri, na msaada endelevu na tumaini
kwa biashara nzuri Zaidi mwaka ujao.
Wauzaji walishukuru juhudi za Hauwei
katika kuboresha kiwango cha ubora cha simu na walikiri ubora wa hali ya juu ya
simu za Huawei zenye marejesho ya % 0.02. Pia walitilia mkazo msimamo wa Huawei
katika kutoa simu bora na kuungana mkono na kampeni ya TCRA kuondoa simu zisizo
halisi nchini Tanzania.
Katika mkutano huo Huawei Device
Tanzania walitangaza simu mpya ambazo zitakua sokoni hivi punde kama P9, Mate
8, GR5, GR3, Y6 Pro, Y3 II na Y3 Lite kuhakikisha wateja wote wa Tanzania wana
uwanja mpana wa uchaguzi.
Kuhusu Huawei
Huawei
ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya
wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika
viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na simu za vya mawasiliano vinatumika
katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228
ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500.
Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei
imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi
ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha
inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha simu za vya mawasiliano duniani kote.
Kampuni
ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti
kwa njia ya modemu na simu za vya matumizi ya nyumbani.
Kwa
sasa hivi kampuni ya simu ya Huawei Tanzania inashikilia nafasi ya 2, ikiwa na
22% ya soko la simu za smartphone. (Q1,2016)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)