Pages

ZURI C 41 ILIYOTENGENEZWA KWA AJILI YAKO

C41_Black_web
Kitu kipya cha mawasiliano kimeingia kutoka kampuni ya Zuri. Kitu hicho Zuri C 41, simu yenye uwezo wa hali ya juu na ubora uliothibitika.
C 41 ambayo inasambazwa nchini na kampuni ya Despec, wasambazaji waliothibitishwa wa bidhaa bora za Zuri , ina ukubwa wa inchi 4.0 na display ya WVGA na RAM ya MB 512, ili kuifanya iwe na utendaji wenye uhakika na madhubuti.
Pamoja na uwezo huo ina kamera ambayo ni safi yenye uwezo mkubwa wa kukupa taswira yenye kuvutia na mwonekano bora.
Aidha ina betri yenye nguvu inayodumu muda mrefu na inayokupa uhakika wa kufanya shughuli zako bila kuwa na woga wa simu kuzimika.
Kwa namna yoyote ile hii ndio simu unayostahili kuwa na tuna uhakika utaipenda.
c41 white
Display yake ya FWVGA inaonyesha picha katika uhalisia. Rangi zionekanazo katika picha upigayo ni asili. Teknolojia yake pia inatoa mwanga wa kutosha na kusaidia mtumiaji katika hali ya mwanga mkali wa mchana au usiku.
Mtumiaji wa simu hatakuwa na wasiwasi wa kusoma ujumbe au kutazama picha hata akiwa katika eneo la mwanga mkali.
Simu hii ya kisasa hukufikia kwa rangi mbili, nyeupe na nyeusi na inanyongeza ya ganda la nyuma ndani ya pakiti kwa ajili yako kubadilisha kuendana na mahitaji ya siku yako.
Zuri C 41 yenye mwonekano wa kuvutia inayo uwezo wa kuhifadhi data wa GB 4 pamoja na memory card yenye ujazo wa GB 8 inayokupa nafasi ya kujaza kumbukumbu zako kadri uwezavyo. Uwapo na simu hii unaweza kuongeza ujazo mpaka GB 32.
Watengenezaji wa simu za Zuri wamehakikisha kuwa mtumiaji wa C 41 amepewa kipaumbele. Mtumiaji wa C 41 atapata kinga ya kioo (screen guard) bure. Hii ni kwa usalama wa display ya simu yako. Pia, inakuja na mkebe wa ziada kwa ajili ya usalama wa simu yako, hii huhakikisha simu yako haipati michubuko na mikwaruzo pale uitumiapo.
C41_Black_web
Simu ya C 41 inatumia mfumo endeshaji wa Andoid 5.1 ambayo ni rahisi kutumia na hukupa fursa ya kupakua vidakuzi mbalimbali. Mfumo huu hukupa wewe mtumiaji chaguzi mbalimbali za mitandao ya kijamii pamoja na michezo huku uwezo wake wa RAM 512 ukihakikisha kasi ya ajabu katika utumiaji.
Muundo wa simu ya C 41 ni wa kuvutia ikinakshiwa na urembo wa almasi kuzunguka kamera.
Fremu yake ya chuma inaongeza thamani ya simu katika soko na kuifanya C 41 kuwa simu ambayo kila mtu atapenda kumiliki.
Simu ya zuri C 41 sasa inapatikana madukani kwa bei ya sh 130,000/-. Tembelea madukani ujipatie msisimko wa mawasiliano kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)