Pages

MARIA STOPES YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA JIJI LA MWANZA NA DAR JUU YA UZAZI WA MPANGO

Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi ya Health Promotion Tanzania (HPT), Bw. James Mlali akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Mwandishi wa wandishi na Muandaaji wa vipindi wa habari wa Redio Free Afrika ya Mwanza, Migongo akiuliza swali kwa mwezeshaji wa mafunzo hayo.
Wasimamizi wa Mafunzo hayo kutoka Maria Stopes Tanzania.
Mtaalamu wa uzazi wa mpango, Bi. Shida Masumbi akiwaonyesha waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam moja ya njia mojawapo inayotumika katika uzazi wa mpango.
Mhadhiri wa SJMC- UDSM, Bw. Abdallah Katunzi akitoa mwongozo kwa waandishi wa habari juu ya mafunzo waliyoyapata waweze kuyafanyia kazi ipasavyo.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Citizen, Bernard Lugongo akiuliza maswali. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - Mwanza.
---
Na Cathbert Angelo Kajuna, Mwanza.

ASASI ya Health Promotion Tanzania (HPT) inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango imeiomba Serikali kuongeza bajeti ya uzazi wa mpango ifikie Sh. bilioni sita.

Kauli hiyo imetolewa na Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi hiyo, James Mlali wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuhusu ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango.

Alisema asilimia 27 ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na asilimia 25 wanakosa huduma hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti inayotengwa na Serikali.

Mlali alisema bajeti ikiwa ndogo hata elimu inakuwa ndogo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.

"Bajeti inayotengwa inatakiwa iendane na ongezeko la idadi ya watu kwa kuzingatia upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo ni elimu,afya, na ajira.

"Pia ongezeko hili alizingatie hali ya uchumi kwasababu asilimia 42 ya watoto wamedumaa akili kutokana na ukosefu wa lishe bora," alisema Mlali.

Mtaalamu wa uzazi wa mpango, Shida Masumbi alisema kuna njia tatu za uzazi wa mpango ambazo ni njia ya muda mfupi, muda mrefu na njia ya kudumu.

Alisema njia za muda mrefu ni kitanzi, kipandikizi na njiti, njia za muda mfupi ni sindano, vidonge na kondomu.

"Pia ipo njia ya kudumu ya uzazi wa mpango ambayo ni mume na mke kufunga kizazi.

"Baadhi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango husababisha maudhi kwa kukosa hedhi, kuongezeka siku za hedhi au kuona matone madogomadogo ya damu,"alisema Masumbi.

Alisema pamoja na maudhi hayo lakini kuna faida ambazo ni kuzuia vifo kwa mama na mtoto, mama kupumnzika kwa muda mrefu na kujishughulisha na kazi nyingine za kimaendeleo.

Masumbi alisema mwitikio wa matumizi ya uzazi wa mpango ni mkubwa na wanaume 300 walijitokeza kufunga kizazi kwa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)