Wauguzi wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiendelea na kazi za mikono.
Mmiliki wa Blog ya Kajunason akimsaidia kusuka kikapu mmoja ya wazee anayelelewa katika kituo hicho.
Moja ya nyumba wanayoishi wazee hao.
Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliotembelea Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi wakifanya mahojiano ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili ambapo wazee hao walisema jambo kubwa linalowaumiza kicha ni upatikanaji wa matibabu katika zahanati yao jambo linalowafanya wengine kuishi na maradhi kwa muda mrefu.
Waaandishi wakiendelea kufanya mahojiano na Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi.
Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza, Michael Bundala akifanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo katika mahojiano hayo alielezea kuwa kuna changamoto nyingi za kuishi na wazee hawa kama kiongozi kwa vile wazee wamekuwa wakorofi mno na kuona siwatendei haki katika maamuzi ambayo nimekuwa nikiyatoa ikiwemo katika ugawaji wa vyakula.
---
Na Cathbert Kajuna - Mwanza.
Wazee wanaoishi katika kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaiomba Serikali kuwapatia huduma za afya katika Zahanati ya kituo chao.
Wazee hao wanaeleza kwamba changamoto hizo katika ziara ya waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliounganishwa pamoja na kuratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) na Marie Stopes Tanzania.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazee hao wanasema katika zahanati hiyo hakuna dawa na wanapoumwa wanalazimika kununua dawa.
Mwenyekiti wa kambi hiyo, Helen Emmanuel anasema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za huduma ya afya pamoja na wenzao wasiojiweza kufukuzwa kambini.
"Tunapofika katika zahanati hii daktari anatupima vizuri lakini hakuna dawa hivyo anatuandikia kwenye karatasi anatuambia tukanunue.
"Kwakweli hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwasababu wakati mwingine tunapoandikiwa dawa hela ya kununulia tunakosa hali inayosababisha tunaendelea kuumia kutokana na kwamba afya zetu ndio hizi na hatuna sehemu ya kujipatia kipato" alisema Heleni.
Pia alisema kwa sasa wapo wazee 78 katika kambi hiyo lakini wapo walemavu wenzao saba ambao wameambiwa wahame kambini waende vijijini wakati hawana uwezo.
"Kwakweli inaumiza sana kwasababu hawana uwezo wa kujitafutia pia mimi sina uwezo wa kuwasaidia kwasababu mimi mwenyewe ni mlemavu ,"alisema.
Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza,Michael Bundala alisema hapa kambini tuna watoto 17 ambao wazazi wao wako humu kambini na wengine waliotimiza miaka 18 tuliwapunguza na kuwatengea eneo kwa ajili ya makazi na tusingefanya hivyo tungekuwa zaidi ya 800 kwasababu wengine wanapeana mimba wenyewe kwa wenyewe.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya, Sebastian Kisumu alisema ipo changamoto ya vijana wa nje kuwapa mimba wasichana wa kambi hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)