Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao . |
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.
|
Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya)
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo amesema
tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko katika kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine , walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa eneo hilo la Matundasi Chunya..
Kamanda Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi
kwenye chumba cha mochwari katika hospitali ya wilaya ya Chunya , majina na makazi yao bado hayajajulikana. Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio. “Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Matondo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761. AFS aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo
.
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza kurusha risasi hovyo hewani ambapo jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa kutoroka . Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi lilianzisha msako usiku huo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili ambao huku wengine wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu hao. Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 ikiwa na risasi 27 kwenye magazine. Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana pamoja na panga .
Mwambelo alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika hospital ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao kwani majina yao bado hayajatambulika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)