Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore ,akiwahutubia wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye matembezi hayo.
wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye matembezi ya Siku ya Malaria wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore wakati wa matembezi ya Siku ya Malaria
Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL Group wakijiandikisha kushiriki katika matembezi ya kuadhimisha siku ya Malaria.
Baadhi ya washiriki wa matembezi ya Kilomita Tano, wakigawiwa Kinywaji cha Grand Malt
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayila (kulia) akiongoza maandamano hayo.
Wafanyakazi wa TBL Group mwishoni mwa wiki walishiriki katika matembezi ya siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika jijini Dar e salaam na kushirikisha serikali, makampuni , mashirika mbalimbali ya serikali na yasio ya kiserikali na wadau wengine wa sekta ya afya.
Matembezi hayo ya kilometa tano yalianzia katika viwanja vya Green vilivyopo Oysterbay na kumalizikia katika uwanja huo
TBL ni miongoni mwa makampuni ambayo yana lengo la kuziwezesha sekta binafsi kuhimiza kuzuia na kutoa huduma za matibabu za Malaria na kuwa na maono ya kuitokomeza kabisa.
Mratibu wa mpango wa Afya Bora wa TBL Group,Julieth Mgani amesema kuwa wameshiriki matembezi hayo Malaria ni moja ya vipaumbele vilivyopo kwenye mpango wa kampuni na dhamira kuu na maono ya kampuni ni kutokuwa na maambukizi ya Malaria kabisa ifikapo mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)