Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (kulia) akikabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Sinza, Parestina, Bi. Agness Mgaya (kushoto) baadhi ya seti za vifaa vya kujifungulia kwa wajawazito. Katikati akishuhudia ni Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Sinza, Dk. Kayola Chrispin. Jumla ya Seti 100 za vifaa hivyo zilitolewa na Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kitengo cha Biashara jijini Dar es salaam na kugawiwa kwa wahusika.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (kulia) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Sinza, Dk. Kayola Chrispin (wa pili kulia mbele) sehemu ya seti za vifaa vya kujifungulia kwa wajawazito. Jumla ya Seti 100 za vifaa hivyo zilitolewa na Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kitengo cha Biashara jijini Dar es salaam na kugawiwa kwa wahusika.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kitengo cha Hazina wakiwa wamebeba sehemu ya misaada waliotoa katika Wodi 'A' ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ichaji wa Wodi 'A' ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Sista Devota Ndendeje (kulia) akiwashukuru sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Kitengo cha Hazina mara baada ya kukabidhi misaada na zawadi kwa wagonjwa walipotembelea wodi hiyo. Miongoni mwa misaada iliyotolewa ni pamoja na mashine ya kumsaidia mtoto anayeshindwa kupumua vizuri (Suction Machine), ENT Seti mbili kwa ajili ya vipimo vya masikio, koo na pua kwa watoto, mashine ya kuwasaidia watoto wenye pumu (Nebulizer machine), Digital thermometer 14, pampers, sabuni, mafuta ya vaseline, cotton buds, miswaki na dawa za miswaki, toilet papers, chupa za maziwa kwa watoto wachanga na zawadi nyingine kwa watoto kama pipi, juice, biscuits na chama.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Hazina wa jijini Dar es Salaam wakikabidhi baadhi ya misaada kwa Ichaji wa Wodi 'A' ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Sista Devota Ndendeje walipotembelea wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili juzi.
-





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)