
Christina Lissu Enzi za Uhai wake
Dada wa Mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan Dar.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana. Taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu tutaendelea kuwajuza na kuwataarifu.
Lukaza blog inapenda kutoa pole kwa familia ya Marehemu Christina Lissu pamoja na kwa Mbunge Mh Tundu Lissu kwa kuondokewa na dada yake. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
Amen





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)