Pages

MULTICHOICE TANZANIA WATANGAZA WASHINDI WA "JISHINDIE NA DSTV"

Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.

Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.

Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.

“Washindi wawili ambao kila mmoja atapata nafasi ya kupelekwa Zanzibar na kukaa huko kwa siku mbili katika hoteli huku akilipiwa kila kitu kuanzia usafiri, malazi, chakula yeye na familia yake ikiwemo baba, mama na watoto wawili. Washini hao ni Mwelly Nyakusaima ambaye ni mkazi wa Igoma-Mwanza na mshindi mwingine ni Evarist Ndambo mkazi wa Tabataa Jijini Dar es Salaam.” Alisema Bi. Hilda Nakajumo.

Aidha, alibainisha kuwa, washindi wengine waliojishindia droo hiyo ambao ni wa kipengele cha pili ni wale wateja ambao tayari walishajiunga na DSTV huku wakitakiwa wasikatiwe malipo yao kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu.

Ambapo wateja 50 wamejishindia DSTV EXPLORA Decoders huku wateja 90 wao wakibahatika kupata kuunganishwa malipo ya bure ya mwezi ikiwemo ya mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita na miezi 12 bure.

Aidha, washindi hao wote walioshinda MultiChoice ilibainisha kuwa, watapigiwa simu na kuelekezwa namna ya kuchukua zawadi zao hizo kuanzia sasa kwa muda hadi June mwaka huu.

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu aliwakumbusha wateja wa DSTV kuendelea kulipia malipo ya ving’amuzi vyao huku wakitoa ofa mbalimbali sambamba na vipindi vizuri ikiwemo vya uhondo wa soka la kimataifa, filamu na muziki..
Tazama MO tv, kuona habari hiyo hapa:

bmn2.0-620x308Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV
DSC_1452Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo akichanganya droo hiyo kwa njia ya kielektoniki kupitia kompyuta. wengine wanaoshuhudia ni maafisa wa MultiChoice Tanzania. Kulia ni mwakilishi kutoka Bahati Nasibu ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Millao.
DSC_1453Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akihakiki moja ya majina ambayo yameingia kwenye droo ya ushindi kwa wateja wa DSTV
DSC_1463Droo hiyo ikiendelea
DSC_1451Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo
DSC_1484Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)