Pages

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF), WATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam
Aprili 19, 2016. Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao
juu ya shughuli za Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo
patatokea madhara awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege, (Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J. Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).
 NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kuwalipia michango ya mwezi.

Semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege. Katika hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na majanga wakiwa kazini.

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008. Akiwakaribisha wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba
alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa
wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu wa kutoa michango kwa wakati 
 Mshiriki akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF
Bi. Pendo Berege, akifungua semina hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba
 Bi. Irene Isaka
 Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani
 Bw. Chakoma (kushoto), akibadilihana mawazo na Bi. Pendo Berege
 Bi Amina Likungwala kutoka WCF, akitoa mada kuhusu wajibu wa vyama vya wafanyakazi
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akitoa mada "Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF)
 Bi. Pendo Z.Berege, (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Ukauzi wa ndani cha Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).Peter J. Mbelwa, wakiteta jambo
 Majadiliano yakiendelea
 Mmoja wa washiriki wa semina akizungumza kwenye kipindi cha majadiliano cha semina hiyo
 Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakichykua taarifa muhimu
Mshiriki akifuatilia kwa makini

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)