Na Magreth Kinabo- Maelezo.
Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) umetoa ufafanuzi kuhusu matibabu ya wagonjwa wa Selimundu(Sickle cell) ambapo umesema kwamba hudumma hiyo haijasitishwa kama ilivyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Ufafanuzi huo, umetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel Eligaesha kuupitia taarifa kwa vyombo vya habari ,ambapo amesema uongozi wa hospitali hiyo haina mpango wa kusitisha huduma hiyo.
“Watu wanaoeneza uvumi huo kuwa huduma hii imesitishwa wana maslahi yao binafsi kuhusu tiba ya wagonjwa hawa,” alisema Eligaisha.
Aliongeza kwamba ni kweli huduma hiyo imekuwa ikitolewa kwa kipindi cha miaka kumi, hivyo kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu ya pamoja na utafiti wagonjwa wa Selimundu, ambao muda wake umeisha 31 Machi, mwaka huu kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote kuja muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba.
Mkuu huyo alisema hivyo basi hali hii ilisababisha wanaohitaji huduma ya selimundu kufuata matibabu hospitalini hapo, licha ya kwamba mahitahi yao hayakuhitaji wataalamu wa MNH.
“ Tunaomba jamii ikumbuke kabla ya mradi huo, hospitali hiyo ilikuwa inatibu wagnjwa hao waliokuwa wanapata rufaa, hivyo baada ya mradi huo kuisha hospitali hiyo imewaagiza wagonjwa hao kufuata mfumo wa kawaida kama ilivyo kwa wagonjwa wengine. Hii ina maana kwamba wagonjwa hao wasiohitaji wataalamu wetu wattaendelea na huduma katika hospitali zilizo karibu nao na watakao onwa na Muhimbili ni wale watakaopata rufaa kutokana na matatizo yao,” alisisitiza.
Aidha Eligaesha alisema wagonjwa hao wanaohitaji huduma yao watapata huduma za matibabu kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo bila ya ubaguzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)