Mke wa Rais Obama kuonekana katika Epsiode ya NCIS itakayorushwa May 3 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

Mke wa Rais Obama kuonekana katika Epsiode ya NCIS itakayorushwa May 3

michelle
First Lady wa Marekani, Michelle Obama akiwakaribisha ikulu Special Agent Leroy Jethro Gibbs (Mark Harmon) na mmoja wa Mke wa Askari wa Kikosi cha Maji aliyejiunga katika kikosi cha maji.

Kwa wale wapenzi wa Series au Tamthilia ya NCIS Los Angelos wataweza kumuona The First Lady wa Taifa la Marekani, Bi Michelle Obama katika episode itakayorushwa tarehe 3 May 2016.

Mke wa Rais Obama wa Marekani, Bi Michelle Obama ataonekana katika episode hiyo akiwa ndani ya White House akiigiza kama mmoja wa wanaharakati anaotoa moyo na kusapoti maisha ya wanajeshi na familia zao kwa kuongeza nafasi za elimu, rasilimali kazi na mipango ya maisha bora.

Katika Episode hiyo iliyochezwa katika Ikulu ya Marekani (White House) Huku Bi Michelle Obama akiwa kama the First Lady ataonekana akimkaribisha Special Agent, Leroy Jethro Gibbs (Mark Harmon) na mmoja wa Mke wa Askari wa Kikosi cha Maji aliyejiunga katika kikosi hiko katika Majadiliano yatakayokuwa yakifanyika ndani ya Ikulu. Huku waigizaji wa ziada katika kipande hiko wakiwa ni wake wa wanajeshi.

Episode ya The First lady Obama ya NCIS ijulikanayo kama Homefront itarushwa Jumanne May 3 kuanzia saa 2 Usiku kwa masaa ya ET kupitia channel ya CBS


UNAHITAJI STORY ZAIDI? Tufollow katika Facebook Lukaza Blog, Insta: LukazaBlog, Twitter: Lukaza2010 na Youtube MultiLukaza Blog kwa kupata habari motomoto na latest kuhusu filamu, tv na muziki na mengineyo.

Kama imekukuna unaweza share na washikaji zako popote pale iwe Facebook, Twitter, Instagram na Hata Kwenye Whatsapp

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages