Pages

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO.

Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi akizungumza baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya kutembelea kata hiyo kutizama athari zilizotokana na mafuriko.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kahe wakiwa katika kikao na ujumbe wa Mbunge wa jimbo la Vunjo uliofika katika kata hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa chakula.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya  Moshi,Michael Kilawila akizungumza na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Kahe waliofikwa na maafa yaliyotokana na mafuriko.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akizungumza na wakazi wa kata ya Kahe baada kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mafuriko.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika kikao hicho kilicho fanyika ofisi ya kata ya Kahe ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini ,Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya,kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.
Mbunge wa Viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akitoa salamau za pole kwa wakazi wa kata za Mabogini na Kahe walioathirika na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya Msaada uliotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akikabidhi mfuko wa Unga kwa baadhi ya wazee katika kata ya Kahe walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akikabidhi Chumvi kwa baadhi ya wazee walioathirika na mafuriko .
Wananchi katika kata ya Kahe wakifurahia pamoja na Wabunge James Mbatia na Lucy Owenya msaada uliotolewa kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)