Meneja wa kuendeleza masoko ya Coca-Cola nchini Mouren Sikka akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya Onja Msisimko
Burudani za kila aina zilikuwepo za kucheza michezo mbalimbali ufukweni,kuogelea na burudani ya muziki
Zawadi mbalimbali pia zilitolewa
Baadhi ya waalikwa wakifurahi kwa kupiga picha kwa mapozi mbalimbali
Wageni waalikwa wakifuatilia burudani mbalimbali katika hafla hiyo
Burudani za kila aina zilikuwepo ndani ya nyumba
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kupata burudani
Wageni wakipata chakula katika hafla hiyo
kulikuwepo wageni wa rika zote vijana kwa wazee
Kampuni ya Coca-Cola imezindua promosheni mpya nchini ya “Onja Msisimko’ jana , hafla kubwa ya uzinduzi ilifanyika katika hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Hafla ya uzinduzi ilisheheni burudani za kila aina ikiwemo muziki kutoka wanamuziki nguli wanaotamba kwa kupiga muziki wa kizazi kipya ambao waliwapatia raha waliohudhuria uzinduzi huo hususani vijana ambao walihudhuria kwa wingi.
Akiongea kuhusiana na kampeni hii, mmoja wa maafisa wa Coca Cola nchini Mariam Sezinga alisema kuwa “Onja Msisimko” ni kampeni inayowapatia watumiaji wa kinywaji cha Coca-Cola kupata fursa ya kuelezea uzoefu na furaha wanayoipata kutokana na kutumia kinywaji hiki.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)