April 5 Watanzania kuanza kuletewa huduma ya Posta Mlangoni - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

April 5 Watanzania kuanza kuletewa huduma ya Posta Mlangoni

 Kaimu Posta Master Mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (hawapo pichani)kuhusiana na Shirika hilo kufungua huduma ya POSTA MLANGONI huduma hiyo itazinduliwa April 5, mwaka huu. Kustoto ni Meneja mkuu wa rasilimali za shirika la Posta Tanzania, James Sando.
 Kaimu Posta Master Mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, (hawapo pichani)Kustoto ni Meneja mkuu wa rasilimali za shirika la Posta Tanzania, James Sando na Kulia ni Kaimu Meneja mkuu wa biashara katika shirika la Posta Tanzania, Janet Msofe.
Baadhi ya wa wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika mkutano na Kaimu Posta Master Mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga wakati akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

SHIRIKA la Posta Tanzania linatarajia kuzindua huduma  mpya POSTA MLANGONI ambapo kila mwananchi atapelekewa kufurushi, taarifa au bidhaa zilizotumwa kwa kupitia Ofisi za Posta.

Hayo yamesemwa na  Kaimu Posta Master Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Shirika hilo litaanza na kata 48 ya Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar Unguja kata 2 na Pemba kata 4.

Kapinga amesema kuwa kata za Tanzania bara zilizopo katika jiji la Arusha ni 8 Mkoa wa Dodoma ni kata 8 na jijini Dar es Salaam ni kata 32.

''Tumeanza na kata 48 kwa kuwa kata hizo zimekamilika miundombinu yake" amesema  Kapinga.

Amesema kuwa awamu ya kwanza itaanza hapo April 5 na awamu ya Pili itakuwa katika mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mara, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Pwani, Manyara, Simiyu na Geita kwa upande wa Tanzania visiwani itakuwa ni Unguja na Pemba.

Na awamu ya Tatu watamalizia na mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Kigoma, Singida, Rukwa, Ruvuma, Katavi na Njombe amesema kuwa shirika la Posta Tanzania lina masanduku 173,000 yaliyosimikwa na shirika hilo na ofisi 172.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages