Pages

Waziri Nape apiga ‘stop’ tiketi za TFF, ataka malipo ya kieletroniki uwanja wa Taifa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye ametoa agizo rasmi juu ya matumizi ya tiketi za Kielekroniki michezoni kwa kulitaka Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuakikisha linatumia tiketi hizo kuanzia Machi 9.2016 na kuachana na tiketi za kawaida huku akibainisha kuwa wataendelea kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu na hatua zaidi ilikuziba mianya ya udanganyifu.

Nape amebainishahayo muda huu wakati anazungumza na vyombo vya habari kuelezea suala la Michezo hapa nchini ikiwemo suala hilo la mfumo wa malipo kwa njia ya Kielekroniki ambapo awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo la matumizi ya mfumo huo.

Akielezea suala hilo, amesema litaondoa ‘figisufigsu’ za mara kwa mara ambazo watu wamekuwa wakilalamikia mapato ikiwemo hayo ya Uwanja wa Taifa.

“Baada ya Machi 8 mwaka huu. Mechi zote zitakazochezwa uwanja wa Taifa, tiketi zote zitatumika ni zile za kieletroniki. Hii ni mara baada ya michezo yote mitatu iliyobaki ambayo TFF wanamalizia tiketi zao ambazo wamebazibakisha na zinaisha Machi 8. Safari hii tutafuatilia na kukagua wenyewe. Hatutakubali kuendelea kuvumilia hujuma katika hili.” Ameeleza Nape katika mkutano huo.
Tazama MO tv hapa kushuhudia habari hiyo:

Na Andrew Chale,modewjiblog
NapeWaziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (Kulia) akizungumza na mwanahabari (Hawapo pichani) wakati akitoa tamko hilo muda huu juu ya kuitaka TFF, kuakikisha inatumia mfumo wa malipo ya Kielekroniki kuanzia Machi 9 na kuendelea kwa michezo yote ndani ya Uwanja wa Taifa huku akielezea kuwa wataendelea kufuatilia ilikubaini udanganyifu zaidi katika suala la mapato la milangoni katika michezo yote. (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)