Pages

Serikali yampongeza Bondia Francis Cheka kwa ushindi wake, yamkabidhi cheti

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamepongeza juhudi za wanamichezo wa Tanzania wanavyoiwakilisha vyema Tanzania hasa katika mambo mbalimbali ikiwemo Michezo kama alivyofanya Bondia Francis Cheka.

Akitoa pongezi hizo mapema leo, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na bondia huyo pamoja na viongozi wa soka akiwemo Rais wa chama cha Ngumi pamoja na Promota wa bondia huyo, Waziri Nape ameelezea kuwa kadri wanamichezo wanavyofanya vizuri ndiyo wanavyoendelea kuipa sifa kemkem nchi hivyo wataendelea kushirikiana nao.

Mbali na kumpongeza bondia, Francis Cheka, Waziri Nape pia alimpongeza mdogo wa bondia huyo Francis Cheka, Cosmas Cheka ambaye naye aliambatana na msafara huo ambapo katika pambano lake naye alishinda mkanda wa WBF, kwa pointi dhidi ya mpinzani wake.
Aidha, Waziri Nape alimkabidhi cheti cha shukrani bondia, Cheka kama ishara ya kutambua mchango wake huo na kuiletea heshima Taifa kwa ushindi wake.
Bondia, Francis Cheka katika pambano lake hilo, alipigana na Raia wa Serbi anayeishi Marekani, Bondia, Geard Ajetovic ambapo katika pambano lao hilo, lililofanyika jijini Dar es Salaam, Cheka alishinda kwa pointi.

Ubingwa huo alioshinda Bondia Francis Cheka, ni Ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF).
Tazama MO tv, kuona habari hiyo hapa:

Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv
bondia chekaBondia Francis Cheka akizungumza na wanahabari mapema leo (hawapo pichani) wakati walipomtembelea Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye ofisini kwake jijini Dar es Salaam. kushoto kwake ni Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi'.
bondia cheka na NapeWaziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye (kulia) akiangalia kwa makini mkanda wa ubingwa wa bondia Francis Cheka. Wengine wanaoshuhudia ni Bondia mwenye Francis Cheka, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' na Promota wa Francis Cheka, Juma Ndambile
bondiaWaziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini wakati wa kupokea shukrani kutoka kwa bondia Francis Cheka (katikati) aliyekuwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mapema leo. kushoto ni Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi'
bondia napeWaziri wa Habari, Nape akijaribisha kuvaa mkanda wa ubingwa wa Bondia Francis Cheka kama ishara ya kumfikishia na kuuvaa kwa niaba ya watanzania wote..
bondia cheka 1Waziri Nape (katikati) akimpa mkono wa pongezi bondia Cosmas Cheka ambaye ni mdogo wa bondia Francis Cheka ambaye naye alishinda katika pambano lake la WBF.
bondi cheka.."Hongera kwa ubingwa Francis Cheka".. Waziri Nape akimpa mkono wa hongera bondia Francis Cheka wakati wa pongezi hizo mapema leo Machi 4.2016
bondia Cheka4Waziri Nape akimkabidhi cheti cha shukrani bondia Francis Cheka kama ishara ya kupokea mchango wake hadi kuitangza na kuiletea heshima kubwa nchi ya Tanzania. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)