Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwarudishia fedha zao
kesho Jumanne, wapenzi wa mpira wa miguu waliokuwa wameshakata tiketi za
kushuhudia mchezo wa kundi G kati ya Tanzania v Chad jijini Dar es
salaam.
TFF
inawaomba washabiki wa mpira wa miguu waliokua wamekata tiketi za
mchezo huo, kufika kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi katika vituo
walivyonunulia wakiwa na tiketi zao ili waweze kurudishiwa fedha zao.
Zoezi
la kuwarudishia fedha washabiki waliokuwa wameshakata tiketi za mchezo
kati ya Tanzania v Chad litafanyika katika vituo vinne vilivyokua
vikiuza tiketi siku ya Jumapili, hivyo wenye tiketi za mchezo huo
wanaombwa kufika na tiketi zao ili waweza kurudishiwa fedha zao.
Aidha
TFF inawaomba radhi watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu kwa
usumbufu uliojitokeza na kuwataka kuwa watulivu na wavumilivu katika
kipindi hiki ambacho wanasubiria taarifa zaidi kutoka CAF.
Chad
imejiondoa jana katika kinyanganyiro cha kuwania kufuzu kwa Fainali za
Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) nchini Gabon mwaka 2017, ambapo iliku
kundi G na timu za Misri, Nigeria pamoja na Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)