Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa hotuba katika mdahalo kuhusu wanawake na uzinduzi wa Kundi la `HeForShe`.
Umoja wa Mataifa Wanawake (UN Women) nchini umefanya uzinduzi wa kundi la mshikamano la Kimataifa linalohusisha wanaume na wavulana lililo na malengo ya kuhakikisha kunapatikana usawa wa kijinsia baina ya wanaume na wanawake ‘HeForShe’.
Akizindua kundi hilo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema usawa kijinsia ni haki ya kila binadamu na kupitia kundi hilo ni wajibu wa kila mwanaume na mvulana kusaidia kupatikana kwa usawa kwa wanaume na wanawake katika maeneo yote ambayo yanaonekana kuwa na upendeleo kwa upande mmoja.
“Usawa wa kijinsia sio tu suala la wanawake pekee, ni suala la haki za binadamu ambalo hutuathiri sisi sote. Usawa wa kijinsia sio tu kuwawezesha wanawake, lakini pia huweka huru watu kutoka katika ubaguzi uliowekwa kijamii na majukumu ya kijinsia,” alisema Rodriguez.
Awali Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt alieleza kuwa usawa wa kijinsia unahusisha pia katika kusimamia shughuli mbalimbali ikiwepo za nyumbani kwa wanaume na wanawake kushirikiana kuzifanya kwa pamoja.
Alisema ni muhimu kwa jamii kuelewa kuwa ni jambo lenye maana kuwepo kwa usawa wa kijinsia ili wanawake nao waweze kusaidia shughuli za maendeleo kwa familia na taifa kwa ujumla.
“Usawa uwepo katika sehemu zote hata kazi za nyumbani zifanyike kwa pamoja … ni muhimu kwa mama, baba na kijana kuwepo kwa usawa wa kijinsia kwa watu wote,” alisema Bi. Rangnitt.
Siku ya Wanawake kwa mwaka huu kidunia imekuwa na kauli mbiu ya kimataifa isemayo ‘Dunia 50-50 Ongeza Jitihada kwa ajili ya Usawa wa Kijinsia’ na kitaifa kaulimbiu imekuwa ni ’50-50 ifikapo 2030 Tuongeze Jitihada’.
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa kwanza kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua Kundi la Mshikamano la `HeForShe`.
Mdahalo ukiendelea, (wa kwanza kulia) Katibu Mkuu wa Bazara Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa wa Wanawake ya Uwezeshaji Kiuchumi, Mehjabeen Alarakhia na Mshauri wa Jinsia na Maendeleo, Edward Mhina.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa hotuba katika mdahalo kuhusu wanawake na uzinduzi wa Kundi la `HeForShe`.
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt.akitoa hotuba kuhusiana Siku ya Wanawake.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk
Mshereheshaji wa mdahalo huo, Usu Mallya
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake nchini, Anna Collins-Falk akikata keki ya kusherekea Siku ya Wanawake Duniani, Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)