Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kampuni hiyo kutoa sh.300 milioni kudhamini masomo kwa wanafunzi tisa wa Tehama vyuo vikuu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi George Mulamula.
Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi George Mulamula (kulia), akizungumza katika mkutano huo.Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (kulia), akiteta jambo na Meneja wa Huduma za Jamii wa Tigo, Woinde Shisael katika mkutano huo.
Mwanafunzi, Carolyne Paul (kulia), atakayenufaika na ufadhili huo akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Magilatech, Godfrey Magila (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Magila ni mtaalamu wa Tehama.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (katikati), na viongozi wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliopata udhamini huo wa sh.milioni 300.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo wametangaza kudhamini wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa kwa jumla ya shilingi million 310.
Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema fedha hizo zitagharamia ada ya chuo, gharama za kufanya utafiti, malazi na chakula kwa kipindi cha miaka minne cha masomo ya Tehama kwa kila mwanafunzi.
Gutierrez amesema udhamini huo unaowalenga kuwasiadia vijana wenye vipaji katika taaluma ya Tehama kutimiza ndoto zao za kimaisha ni sehemu ya sera ya kampuni hiyo ya mawasiliano ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kukuza sekta ya tehama na kuleta maendeleo nchini.
“Tunaamini kupitia udhamini huu kampuni yetu, kwa kushirikiana na DTBi, inatoa mchango wake katika kujenga kizazi kijacho cha mabingwa katika sekta ya Tehama ambao watakuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi hii,”Gutierrez amesema akiongeza kwamba tayari kuna makubaliano kati ya Tigo na DTBi unaowapa wanafunzi kutoka DTBi fursa ya kubuni bidhaa mbalimbali vya Tehama ambavyo hutumiwa na Tigo kibiashara na mapato kugawanywa kwa wadau wote.
Wanafunzi tisa waliobahatika kupata udhamini wa Tigo ni Erickson Muyungi (UDSM), Fatma Moshi (UDSM), Caroline Paul (UDSM), Michael Lunyungu (UDOM), Robert Charles (UDOM), Isack Kipako (UDOM), Jacqueline Dismas (UDSM), Jumanne R. Mtambalike (IFM) na Joel Mtebe (UDSM).
Akizingumzia zaidi kuhusu mkataba huo kati ya Tigo na DTBi, Mkurugenzi huyo wa Tigo amesema: “mbali na udhamini tunaoutoa kwa wanafunzi wa Tehama tuna mradi wa pamoja uitwao ‘Project Digitize’ ambao umewawezesha wanaTehama chipukizi kuanzisha kampuni zao kuipitia ubunifu wao na ambao wanapata msaada kutoka Tigo katika kuendeleza miradi yao. Hadi leo kuna wanatehama watatu wanaosaidiwa na Tigo kupitia mpango na ambao bidhaa pindi bidhaa zao zitakapoanza kutumika kibiashara, watafaidika kutokana na mgawanyo wa mapato..”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi Mhandisi George Mulamula kwa upande wake amesema üshirikiano na Tigo umetoa fursa na njia za kibunifu kwa wanafunzi wa DTBi kupata elimu, kujenga uwezo wao wa Tehama ambavyo vitawasaidia kuonyesha vipaji vyao katika fani hii ndani na nje ya nchi.”
Mulamula aliongeza kusema kwamba: “DTBi’s ina malengo ya kuwahamasisha vijana wakiwemo wanawake kujenga tabia za kuwa wajasiriamali Tehama ili kusaidia kukuza sekta binafsi na kuongeza makusanyo ya kodi nchini. Katika kutekeleza azma hii, Tigo imetoa mchango mkubwa kwa kuwawezesha wajasiriamali wetu kufikia ndoto zao za uzalishaji mali, kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, kuleta nafasi mpya za ajira yote haya yakiwa ni vielelezo vya jinsi ambavyo tehama inaweza kusaidia kukuza pato la Taifa kwa ujumla.”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)