Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa kufungua rasmi semina maalum kwa vijana wapatao 500 wa shule za Sekondari zikiwemo za Turiani Sekondari, Makurumla na zinginezo za Manispaa ya Kinondoni pamoja na walezi na walimu, ambapo katika mkutano huo, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, juhudi zinazofanywa na Mwanadada Millen Magese ni za kuungwa mkono hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, anatambua wanawake wengi duniani kote wanasumbuliwa na tatizo hilo ambapo gharama zake kwa kawaida ni kubwa huku bado wataalam wanaendelea kushughulikia namna ya upatikanaji wa tiba yake ili kuweza kuwa nafuu.
“Napongeza juhudi za dhati zinazofanywa na taasisi ya Millen Magese, katika kuunga mkono juhudi za serikali ya tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za kuwasogeza wananchi karibu na huduma bora kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Jamii yetu.
Tatizo la kutoshika mimba (kitaalamu Endomytiosis) hutokana na sababu mbalimbali, nyingi zikichangiwa na uelewa mdogo wa jamii inayomzunguka msichana au mama anayejianadaa kuanza kubeba mimba, lakini pia upungufu wa vifaa tiba hospitalini na kwenye vituo vya afya sambamba na kukosekana kwa wataalamu katika hospitali zetu, Hivyo tunapenda kuchukua fursa hii kupongeza juhudi kama hizi za kuandaa semina na warsha ikiwa ni hatua madhubuti na ya msingi katika kuikabiliana na changamoto ya uelewa wa tatizo hili katika jamii.
Kwani, tunaamini, limekuwa jambo la faraja sana, tangu Magesse alipojitokeza hadharani na kuihabarisha dunia juu ya tatizo hili linalomkabili yeye binafsi. Naomba kusema wazi kuwa, huo ulikuwa uthubutu wa pekee wa mrembo huyo, kiasi cha kuifanya jamii kubwa ya kimataifa kuanza kulifuatilia tatizo hili ili kusaidia mabinti wadogo ambao walikuwa hawajakumbwa na hali hiyo. “ alieleza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla katika hotuba yake hiyo.
Aidha, Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, ni faraja kubwa kwa watanzania tangu Magese Foundation ilipoanzishwa ikifanya kazi kubwa ya kuhamasisha upatikanaji wa vifaa na pia ujenzi wa hospitali maalumu kwa ajili ya kutibu tatizo hilo. Jambo hilo linaendelea kuitia moyo serikali hususani Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufikia lengo la kumuwezesha mtoto wa kike kufikia malengo tarajiwa.
Kwa upande wake, Mwanadada Millen Magese amewaeleza vijana wa kike katika semina hiyo kuwa, wawe wazi pindi wajisikiapo dalili mbalimbali wakati wanapokuwa katika mzunguko wa siku zao ambapo na kubainisha kuwa, jambo hilo endapo litabainika mapema ni rahisi kulipatia tiba kuliko kuficha na kufika steji mbaya.
Mwanadada, Millen Magese pia alitumia wasaha huo kuishukuru Serikali kwa namna walivyokubaliana kushirikiana naye bega kwa bega katika mapambano dhidi ya tatizo hilo hapa nchini ambapo pia amewashukuru wadau wote kwa kuwa naye dhidi ya mapambano hayo.
Semina hiyo pia imeweza kukusanya watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu wasanii, wanamitindo na wabunigu wa mavazi, wafanyabiashara na wanaharakati wanawake katika maendeleo hapa nchini huku wanaume nao wakijumuika pamoja ilikusambaza ujumbe huo kwa wenza wao na marafiki zao.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mwanadada, Millen Happiness Magese (katikati) pamoja na Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa.
Mwanadada, Millen Happiness Magese.
Baadhi ya wanafunzi, wadau wanaosaidiana na mwanadada Millen Magese wakifuatilia semina hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa, wakiwemo waliowahi kushiriki mashindano ya ulimwende hapa nchini ..wakiwa wamejumuika pamoja kuungana na taasisi ya Millen Magese.
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo
Wanafunzi wakifuatilia semina hiyo.
Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rogers Shemwelekwa akitoa hotuba fupi katika semina hiyo
Baadhi ya wadau walioungana kwa pamoja kusaidiana na taasisi ya Millen Magese wakifuatilia semina hiyo. Mustafa Hassanali pamoja na Rio Paul ambao wote ni wabunifu wa mavazi hapa nchini.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,akitoa hutuba yake
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba yake katika semina hiyo.
Mmoja wa madaktari bingwa wa wanawake wa Hospitali ya Muhimbili akitoa maelezo machache .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiendeshwa kwenye semina hiyo..
Mwanadada Doris Mollel ambaye alikuwa akiongoza semina hiyo akieleza machache wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Dk. Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo machache wakati wa kufunga mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mwanadada Millen Happiness Magese wakipata picha ya pamoja na wanafunzi wa shule za Sekondari mara baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na Mwanadada Millen Magese.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wanafunzi hao.
Mwanadada Millen Magese akipata 'Selfie' na wanafunzi pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri Dk. Kigwangalla
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mwanadada Millen Magese wakifurahia jambo na wanafunzi
Mwanadada Millen Magese akipata picha ya 'selfie' na wanafunzi waliojumuika katika semiana hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata picha ya pamoja na waandaaji wa semina hiyo pamoja na wadau wengine kutoka Serikalini. Semina hiyo imefanyika mapema leo Machi 30.2016, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)