Mteja
akipata maelezo kuhusu Simu mpya ya Samsung Galaxy S7 kutoka kwa balozi
wa Samsung Rhoda Iddy (kushoto) siku ya uzinduzi wa Simu hiyo
uliofanyika mlimani city.
Balozi
wa Samsung(kushoto) akimsaidia mteja kuvaa vizuri kifaa cha Gear VR
kutoka siku ya uzinduzi wa Simu mpya ya Samsung Galaxy S7 uliofanyika
mlimani city.
Mteja
akipata maelezo ya Gear VR kutoka kwa balozi wa Samsung(kushoto) siku
ya uzinduzi wa Simu mpya ya Samsung Galaxy S7 uliofanyika mlimani city.
Mteja
akipata maelezo kuhusu Simu mpya ya Samsung Galaxy S7 kutoka kwa balozi
wa Samsung (kushoto) siku ya uzinduzi wa Simu hiyo uliofanyika
mlimani city.
Baada ya mchaka mchaka uliokuwa na
mafanikio makubwa wa kuweka oda za kununua simu za Samsung Galaxy S7, simu hizi
zimezinduliwa rasmi Tanzania mwezi Machi. Kizazi hiki kipya cha Samsung kweye
familia ya bidhaa za Galaxy, simu hizi za galaxy S7 na S7 edge zinaongoza
kwenye sekta hii kwa kuwa na dizaini nzuri, kamera ya kiwango cha juu, program
zenye ubora zilizoungwanishwa na mtandao wa bidhaa na huduma za Galaxy.
Hayo
yote yatakufanya ufikiri upya uwezo wa simu katika utendaji.
Kiongozi katika uvumbuzi wa simu za
mkononi, Samsung imeendelea kuvuka mipaka katika vifaa na huduma, kutengeneza
vifaa ambavyo vinasaidia wateja kupata Zaidi katika maisha yao kwa kuzindua
kizazi cha saba katika Samsung Galaxy, S7 na S7 Edge kwa watanzania. Uzinduzi
rasmi wa Samsung Galaxy S7 na S7 Edge tarehe 19 March umeashiria mwanzo wa
kufikiria namna simu ya mkononi inaweza
fanya kazi ambavyo inaeleza tena namna tunavyofikiria kuhusu teknolojia.
Matarajio na furaha ya kuwa wa kwanza
kuishika na kumiliki simu mpya ya Samsung Galaxy S7 ilishuhudiwa na namba kubwa
ya watu walioweka oda mapema kwa manunuzi yaliyofanyika wiki 2 zilizopita. Simu
hizo zilikabihiwa kwa wateja hao waliokuwa wameweka oda mapema. Pia walipewa
spika za masikioni zinazotumia Bluetooth ambazo zinajulikana kama Samsung level
U.
"Nilisubiria
kwa muda mrefu kununua simu mpya na pale Samsung walipozindua simu yao ya
Galaxy S7 wiki chache zilizopita, nlijua huu ndio wasaa sahihi. Nilikuwa ni
mmoja wa wateja waliojisajili kwa ajili ya oda mapema simu yangu mpya ya
Samsung Galaxy S7. Nilipoishika mikononi mwangu nilishtushwa na kasha jinsi
walivyokuwa wameifungasha kwa ubora wa juu. Tena, shauku niliyojisikia wakati
wa kufungua ina nguvu kama ile ajisikiayo mtu atumiapo bidhaa kwa mara ya
kwanza.” Usemi kutoka kwa Mohamed Musa
Mteja aliyenunua Samsung Galaxy S7 kwenye duka la Samsung Mlimani City. “
Katika Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge, Samsung elektronik imezingatia kuacha
ukumbusho wa ufunguzi wa simu hiyo. Umakini wa ndani haukuwekwa katika
utengenezaji wa simu tu- ufungaji na pakeji pia imefanyiwa mabadiliko” haya
yalielezwa na Rayton Kwembe Meneja
Bidhaa wa Samsung Elektronik Tanzania, akikaribisha watanzania kushiriki
katika uzinduzi
Uzuri wa
simu hii kutoka Samsung ni vile inawapa watumiaji kuhisi vizuri kiganjani mwao
lakini ikiwa na kioo kikubwa. Kava lake la mbele na nyuma lina fiti vizuri
kiganjani. Ina mwonekano mzuri kuitazama kama ilivyo vizuri katika
matumizi.
Wakati wa uzinduzi wa Samsung Galaxy
S7 na S7 Edge, Meneja mkurugenzi wa
Samsung Elektronik Tanzania" Thermoforming
3D ni njia mpya ya kipekee katika maendeleo ya teknolojia na kuchangia uvumbuzi
na ubunifu kama huo ni muhimu. Hatuna nafasi ya kueleza kikamilifu michakato inayohitajika
kuunganisha kioo na chuma , wala hauhitaji kuelewa namna zakiufundi kuelewa
ufanisi wa Galaxy S7 Edge mpya. Unachohitaji ni kushika kifaa na kuhisi tofauti
katika mikono yako ".
“Wateja
waliofanya oda za awali kwa ajili ya Samsung Galaxy S7 na S7 Edge walipewa
kipaumbele kwenda kupokea simu zao mapema kabla ya tarehe 19 Machi. Mauzo ya
simu hii hapa tanzania yanatarajiwa kuvunja rekodi. Kwa kuongeza samsung
imeweka promosheni kwa wateja wote watakao kuwa wananunua simu za samsung
galaxy S7 kuanzia siku hii ya uzinduzi watapewa powe bank ya bure kutoka
samsung na fursa ya kuingia kwenye ndroo ya kila siku ya kujishindia samsung
Gear VR. Simu hii mpya inakuja na kifurushi kutoka vodacom ya 10 GB na bei yake
ni milioni 1.89, Aliongeza Bwana Ibrahim Kombo Meneja Rejareja Samsung Electronics
Tanzania.
Simu
za Samsung Galaxy S7 na S7 edge zinapatikana kwenye maduka yote ya Samsung na
Vodacom nchi nzima.
Kuhusu Kampuni ya vifaa vya
Samsung.
Kampuni ya vifaa vya Samsung ni kiongozi ulimwenguni katika teknolojia,
kufungua fursa mpya kwa watu wote kila mahali. Kwa kupitia teknolojia ya hali
ya juu na ugunduzi mbalimbali, kampuni ya Samsung inahamasisha ulimwengu na
kuleta matumaini ya mabadiliko katika mitazamo na teknolojia zinazolenga katika
televisheni, simu, vifaa vya kuvaa, kamera vifaa vya umeme, mtandao, vifaa vya
afya na LED. Samsung imeajiri zaidi ya wafanyakazi 319,000 katika nchi 84 na
inafanya mauzo ya mwaka dola bilioni 216.7 kujifunza zaidi tembelea www.samsung.com.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)