RC Paul Makonda akabidhiwa Neno la Mungu - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RC Paul Makonda akabidhiwa Neno la Mungu

Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi siku ya jana katika ibada amemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda biblia ya Neno la Mungu kwa makusudi ya kusoma Neno hilo kila siku ili liweze kuwa msaada wake katika shughuli za kila siku za Kiserikali!

Ni siku chache tangu Mh. Rais Magufuri ateue wakuu wa Mikoa nchini,hivyo kwasasa majukumu na upinzani kwake utakuwa mkubwa zaidi na mwanzo,hivyo anamhitaji Mungu sana Alisema Apostle Ndegi.Apostle Ndegi aliongeza kwa kusema Mh. Makonda anahitaji maombi ya kila Mtu kwa Mungu ili afanikishe majukumu yake sawasawa.

Mh.Makonda akiongea alisema kila mtanzania kwa nafasi yake lazima ahakikishe anatimiza majukumu yake vizuri tena kwa kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo kwa nafasi ya mtu mmoja na kuacha kutegemea na kusubiri serikali.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Makonda aliongozana na Mke na Mrisho Mpoto katika Ibada hiyo.
Mh. Paul Makonda alipokuwa akizungumza
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi
Mrisho Mpoto aliongozana na Mh.Paul Makonda 

Apostle Ndegi akieleza jambo kuhusu Mhe Makonda

Mrisho Mpoto aliongozana na Mh.Paul Makonda 
Apostle Ndegi akimpa maelekezo kuhusu kusoma Neno la Mungu kila siku maana ndio litamsaidia katika shughuli za kila siku
RC Paul Makonda akiwa na mke wake wakikabidhiwa Biblia ya Neno la Mungu 
RC Paul Makonda alipata kuongoza nyimbo ya sifa katika ibada hiyo 
RC Paul Makonda alipata kuongoza nyimbo ya sifa katika ibada hiyo  




Apostle Ndegi na wachungaji wengine katika Kanisa hilo wakifanya maombi kwa Mh. Paul Makonda
Picha ya pamoja Apostle wa kwanza kushoto,Mhe Makonda,Mke wa Apostle Ndegi ni mke wa Mh. Makonda Source:gospelhabari.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages