Rebecca Semoka akiwa ofisini kwenye Kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam
Rebecca akionyesha umakini katika kuonja bia kiwandani hapo
Aongoza bara zima la Afrika
Mfanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania katika kiwanda cha
Ilala kilichopo jijini Dar es Salaam Rebecca Semoka, ameshinda tuzo ya kuwa
muonjaji bora wa bia kutoka barani Afrika, katika shindano la kuonja vinywaji
lililoandaliwa na kampuni ya SABMiller na kushirikisha wafanyakazi wake wenye
utaalamu wa kuonja vinywaji kutoka kwenye viwanda vyake vilivyopo sehemu
mbalimbali duniani .
Rebecca ameweza kuwa
mwonjaji bora wa bia kutoka barani Afrika katika shindano hilo ambalo
hufanyika kila mwaka chini ya usimamizi wa kampuni ya kimataifa AROXA inayoshughulika
na usimamizi wa ubora wa bidhaa
zinazozalishwa viwandani . Mwaka
huu shindano hili lilijumuisha washindani kutoka mabara ya
Afrika,Ulaya,Asia,Latin America na Amerika ya Kaskazini.
Akiongea juu ya ushindi alioupata alisema kuwa unatokana na elimu
yake, mafunzo na mazoezi mbalimbali ambayo amekuwa akiyapata katika kampuni anayofanyia kazi ya TBL Group.
“Mimi taaluma yangu nimesomea Sayansi ya Chakula na tekinolojia (Food Science
&Technology) ambayo inajumuisha masuala ya ubora wa vyakula na vinywaji kutoka chuo kikuu
cha kilimo Sokoine. Mafunzo mengi Zaidi kuhusiana na ubora wa bia niliyapata nikiwa kazini hivyo kunifanya
kuwa mtaalamu niliyebobea katika
fani hii ya uonjaji wa bia”.Alisisitiza
Rebecca ambaye anafanya kazi kama mtaalamu wa ubora wa
vinywaji katika kampuni ya TBL alisema kuwa jukumu lake kubwa ni kuhakikisha
bidhaa zinazozalishwa zinakuwa bora na katika mazingira ya usafi ili kutoleta
madhara kwa watumiaji wake ambao ni wateja.
Alisema uonjaji wa bia unafanyika katika viwanda vyote ili
kujiridhisha kuwa bidhaa zinazoingia kwenye masoko ziko vizuri “Pamoja na
kuwepo mashine za kupima ubora na makampuni ya kudhibiti viwango vya ubora wa
bidhaa zetu bado tunahakikisha tunazionja kabla ya kutumiwa na wateja na
uonjaji sio wa ladha tu bali hata
kuzinusa na kuziangalia kwa macho ili kuhakikisha ziko vizuri’.Alisema.
Rebecca alimalizia kwa kusema kuwa anajivunia ushindi huu
kwake binafsi na mwajiri wake “Ushindi huu unadhihirisha kuwa watanzania
tunaweza tukiamua na mfano Dhahiri wa jambo hili ni kwa jinsi viwanda vyetu vya
Mwanza na Mbeya vinavyoshikilia rekodi
ya kuwa viwanda bora barani Afrika ambavyo vinavutia wageni kutoka kwenye hata
nchi zilizoendelea kuja kujifunza jinsi vinavyoendesha kazi zake”.Alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)