Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa
habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za
matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa
kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa
simu feki ifikapo June mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya
huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la
uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika
katika nchi nyingi zilizoendelea.
Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu
kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili
kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.
Meneja
Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa
habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya Huawei,
ambapo wanajitahidi kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza
zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei.
"Ili
kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei
pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es
Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na
kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja
wao kirahisi.jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu ,
Samora jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi
wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye
viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda
sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu
za mkononi za kisasa,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya
pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam, 25 Febuari 2016: Kampuni
ya simu kutoka nchini China ya Huawei, imezidi kutanua wigo wa huduma
kwa kuzindua maduka mawili ya simu moja likiwa jengo la JMall na duka la
pili lenye Kituo cha huduma ya matengenezo ya simu za mkononi likiwa
jengo la NHC karibu na TTCL mtaa wa Samora. .
Hii ikiwa ni baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei jijini
Dar es Salaam na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya uhakika na orijino
vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.kwa ukaribu zaidi jijini la Dar es Salaam.
Maduka hayo ya Huawei yana mahali husika panapo ruhusu wateja wake kuangalia na kujaribu simu na vifaa vingine vya Huawei. Maduka
hayo pia yanatoa nafasi nzuri kwa wateja kupata huduma bora na kuzoea
bidhaa za Huawei na hata kwa kujaribu baadhi ya vifaa vyetu vya mtandao
vyenye uwezo wa 3G/4G LTE Smartphone.
Maisha
ya wateja wetu yana badilika kila siku na matarajio yao ni kuona ubora
na ukuaji wa huduma katika kiwago cha juu zaidi. Kama wadau wakubwa
Huawei imekuwa ikijitahidi katika kukidhi mahitaji ya kila siku ya
wateja na pia kuahidi kuwaonyesha wateja thamani ya pesa yao.
“Dar
es salaam kama kitovu katika ukuaji wa uchumi, tunaamini maduka yetu ya
simu na pia kituo cha matengenezo ya simu za mkononi yataongeza ufanisi
na kusaidia ufikiaji wa huduma za mawasiliano kwa ukaribu Zaidi. Maduka
yetu yamejikita katika ubora wa kutoa bidhaa kwa wateja wa rejareja na
kuwapa wauzaji uwezo wa kupata vifaa halisi, bora na pekee”.
Alisema Mh Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa vifaa vya Huawei.
Maduka mapya ya Huawei, mbali na uuzaji wa Simu za mkonon , Pia yatatoa huduma baada ya mauzo wataalam wa mauzo wataweza watatoa msaada wa kifundi na utumiaji na matengenezo
Katika
kusherekea ufunguzi huu wa maduka ya Huawei na kituo cha huduma za
simu, Huawei inatoa punguzo la bei kuanzia tarehe 25 mpka tarehe 29
mwezi huu ikiwa pamoja na promosheni za simu zao P8 na G8. Manunuzi ya
simu hizi mbili za P8 na G8 yataambatana na zawadi kama selfie stiki,
spika za Bluetooth na tisheti.
Huawei
Tanzania imejipanga kuhakikisha ina weza kuwafikia wateja wake wote
Tanzania kote katika ubora na huduma zenye ufanisi Zaidi.
Maduka
yetu yatakuwa yanatoa huduma itakayo fanya manunuzi yako yawe ya
kihistoria, pia tupo kwenye msimu wa kuhakikisha uwepo wetu unajulikana
Tanzania kwa ujumla kwa kuanza na Dar es salaam” aliongeza meneja wa Huawei nchini.
Maduka hayo yatatoa huduma siku zote za wiki saa 2 asubuhi hadi saa
kumi na moja jioni jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi yatakuwa wazi
kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba mchana.
Maduka
ya Huawei yatakuwa kwa ajili ya kuboresha utumiaji sahihi wa
teknolojia katika njia sahihi zaidi, Wateja Wote mnakaribishwa
Kuhusu Huawei
Huawei
ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa
ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora
katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano
vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika
nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014
kati ya makampuni 500. Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za
kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji
wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani
kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika
kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano duniani kote.
Kampuni
ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za
intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani.
Huawei
imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom,
Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN,
CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom,
NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.
Kupata habari Zaidi tembelea www.huaweidevice.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)