Pages

Mgombea uwakilishi Marekani William Jawando ahojiwa Kilimanjaro Studio, azungumza na Diaspora

Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando, leo alihojiwa katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani ambapo alizungumzia kuhusu mikakati yake katika kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla.

Will, ambaye akishinda atakuwa ni mtu wa pili aliyezaliwa na Baba aliyetoka Afrika kuingia bungeni humo (baada ya Rais Obama) ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ambavyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni muhimu Zaidi nchini Marekani, na hasa kwa wakazi wenye asili ya Afrika waishio vitongoji vya Washington DC.

Ikumbukwe kwamba, inakadiriwa kuwa mmoja kati ya wazaliwa kumi wa Afrika walipo nchini Marekani, anaishi eneo hili, na nusu yao, wameingia nchini baada ya mwaka 2000. Hivyo amefafanua namna ambavyo kuwa na mtu mwenye kuelewa na kuwakilisha vema jamii hiyo, ni muhimu kwa jamii hiyo.

Aligusia pia namna ambavyo asili yake na makuzi yake yamechangia yeye kuingia katika kazi za kuihudumia jamii, akaeleza vipaumbele vyake kwenye uongozi wake ujao na pia wito alionao kwa jamii ya waAfrika walioko Marekani.

Uchaguzi wa kuteuliwa kugombea kupitia chama cha Democrat utafanyika Aprili 26, lakini kura za mapema zitapigwa kati ya Aprili 14 na 21.

Kujua mengi kuhusu Will Jawando, maisha yake, kampeni na mipango yake, tembelea willjawando.com

Anagombea kiti kilichoachwa wazi na mwakilishi Chris Van Hollen ambaye ameamua kugombea kiti cha Seneti kinachoachwa wazi na Seneta Barbara Mikulski anayestaafu

Mahojiano kamili na Will Jawando yatakujia hivi karibuni

Baada ya mahojiano, Will alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wanaDiaspora wa Afrika waliokuwa ndani ya jengo ilipo studio.
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akipata picha na Mubelwa Bandio baada ya mahojiano
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza na baadhi ya waAfrika waliohudhuria "Meet & Greet"
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza na baadhi ya waAfrika waliohudhuria "Meet & Greet"
Michelle Jawando, mke wa mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza machache kuhusu umuhimu wa uchaguzi wa mwaka huu


Mubelwa Bandio akiendelea na maandalizi ya mwisho ya mahojiano na Will Jawando
Mmoja wa wadau wa Kilimanjaro Studio Harieth Shangarai akimpatia maelezo machache Will Jawando
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akiuliza maswali kuhusu uendeshaji wa Kilimanjaro studio
Mubelwa Bandio akitoa maelekezo kwa Will Jawando
Mahojiano yanaendelea

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)