MFUMO DUME NI KIKWAZO CHA WANAWAKE KUTOKUMILIKI ARDHI - ANNA MGHWIRA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MFUMO DUME NI KIKWAZO CHA WANAWAKE KUTOKUMILIKI ARDHI - ANNA MGHWIRA

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira

Na Fredy Njeje-Blogs za Mikoa

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Anna  Mghwira amesema umiliki wa ardhi kwa wanawake hapa nchini bado unasuasua kutokana na mfumo dume uliopandikizwa tokea miaka ya nyuma.

Bi Mghwira ambaye alikuwa mwanamke pekee  aliyegombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 kupitia ACT Wazalendo, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Blogs za Mikoa kuhusu sababu za wanawake wengi nchini kutomiliki raslimali muhimu ya ardhi.


Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 idadi ya  wanawake hapa nchini ni asilimia 51% lakini wanaomiliki ardhi ni  asilimia 19% tuu jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanawake wengi bado hawamiliki ardhi ukilinganisha na wanaume.


''Tatizo lililopo hapa nchini ni tatizo la  kitamaduni, ilikuwa kazi ya mwanamke akishazaliwa ni alelewe na baadaye  akiolewa anaendeleza kizazi huko alikoolewa lakini kumiliki ardhi ni mfumo mpya ambao unatoa fursa sawa katika kumiliki raslimali hiyo muhimu kwa ajili ya kuitumia katika shughuli za kiuchumi''Amesema Mghwira.


Bi Mghwira ameenda mbali zaidi na kuona  tatizo la umiliki wa ardhi pia lipo kwa upande wa wanaume hasa  inapotokea suala la makubaliano na mwekezaji ndiyo maana kuna kesi 


nyingi kuhusiana na wawekezaji na wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Baadhi ya wanaume waliopo katika mmoja ya Kijiji Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakiongea na Blogs za Mikoa kutoa maoni yao ya namna ambavyo walikuwa hawakubaliani na wanawake kumiliki Ardhi


Katika jitihada za kuunga mkono Serikali katika jitihada mbalimbali za kutatua kero kwa wananchi Bi Mghwira  amesema kwamba mara kwa mara amekuwa akielimisha wanawake hapa nchini katika kutambua haki zao na kujikwamua na umasikini.

Hata hivyo ameitaka serikali kutizama upya  sheria ya ardhi na pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na umiliki wa ardhi ili kuwezesha wananchi kutambua kuwa umiliki wa ardhi ni wa haki  kwa pande zote kwa upande wa wanaume na wanawake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages