MADAM SOPHY CHARITY EVENTS YAZINDULIWA RASMI, JAMII YATAKIWA KUSAIDIA WENYE UHITAJI MAALUM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MADAM SOPHY CHARITY EVENTS YAZINDULIWA RASMI, JAMII YATAKIWA KUSAIDIA WENYE UHITAJI MAALUM

mada wote
Baadhi ya wadau wakitoa zawadi na vitu mbalimbali kwa Madam Sophy ambavyo vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu na wale wa Makumbusho Sekondari.
Taasisi mpya ya Kijamii  ijulikanayo Madam Sophy Charity Events yenye malengo ya kusaidia jamii hasa ile yenye uhitaji maalum ikiwemo watu wasiojiweza imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na kutoa misaada mbalimbali kwa watu na watoto wenye uhitaji huo maalum.
Tukio hilo la kipekee lililoandaliwa na kuratibiwa na Mwanadada, Sophia Mbeyela pia lilijumuisha wadau na marafiki mbalimbali walioungana na Madam Sophy katika kufanikisha tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ambayo ilishirikisha watoto wanafunzi wa kituo cha Matumaini wenye Ulemavu wa viungo na ngozi.
Madam Sophy na marafiki zake kwa pamoja waliweza kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watoto hao ambapo pia walipata wasaha wa kuzindua taasisi hiyo huku mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa ambaye aliahidi kufikisha kilio cha walemavu na watu wenye mahitaji maalum Serikalini paamoja na kwenda kuwasilisha Bungeni ilikuona utekelezaji wake kwa ukaribu.
“Madam Sophy Charity. ni taasisi ambayo zaidi ni kuona wenzetu wenye uhitaji maalum hasa walemavu wanapata nafuu katika kuendana na majukumu ya nchi hii kwani sote tuna haki sawa kama wengine na ulemavu wetu usitutenganishe. Tunahitaji Serikali kuhakikisha inashusha bei vifaa vyote vya walemavu ikwemo viungo vya bandia ikiwemo mikono na miguu ambayo kwa kiungo mimoja pekee yake kinakaribia hadi milioni moja” alieleza Madam Sophy.
Madam Sophy aliongeza kuwa, Serikali inayo wajibu wa kujenga shule nyingi zaidi za watu wenye ulemavu kwani zilizopo sasa bado ni chache na watu wenye ulemavu wamehamasika kujitokeza kusoma  hivyo jukumu lililopo ni kuhakikisha wanaongeza shule za watu hao pamoja na kutengeneza miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa walemavu kuanzia mashuleni na hata maeneo muhimu.
Aidha, Kwa upande wake, mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia kiasi cha Sh Laki tano kwa ajili ya kuunga mkono juhudi na harakati za Madam Sophy ambapo alieleza kuwa, licha ya ulemvu wake ameweza kuonesha njia ya kujikwamua pamoja na kuwasaidia wenzake.
Madam Sophy ambaye kitaaluma ni Mwalimu,  ni miongoni mwa wanafunzi waliopata kusoma katika shule hiyo na kumaliza hapo darasa la saba mwaka 2002 ambapo pia aliendelea na shule mbalimbali ikiwemo Sekondari ya Jangwani na baadae chuo, ameomba wadau kujitokeza kuungana naye katika kuhakikisha wanasaidia watu na jamii yenye uhitaji maalum kwani kutoa  ni moyo.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:

madam7
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akitoa nasaha zake kwa niaba ya Mh. Masauni. wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo ya Madam Sophy Charity Events. Upande wa kulia ni Madam Sophy. (Imeandaliwa na Andrew Chale, Modewjiblog)
madah
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Wakovu wanaosimamia shule hiyo ya Msingi wakifuatilia tukio hilo..
madajhj
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika mkutano huo.
madam yy
Wageni waalikwa.
madae
Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wakiwa katika tukio hilo.
madass
Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakitoa burudani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani)
mada
Mtoto Emmanuel Anthony 'Rais' akifurahia jambo katika tukio hilo. Emmanuel ameeleza kuwa, licha ya kuwa mlemavu, ndoto yake ni kuja kuwa Rais.
madahg
Meja wa Wilson Chacha wa Jeshi la Wokovu ambaye pia aliwahi kumfundisha Sophy miaka ya nyuma akitoa salamu zake katika tukio hilo
madam 4
Mtoto akisoma risala maalum kwa mgeni rasmi
madam2
Mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akikata keki kwa pamoja na Madam Sophy kuashiria uzinduzi rasmi wa tukio hilo.
madggf
Mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akimlisha keki Madam Sophy.
madasssss
Madam Sophy akimlisha keki mgeni rasmi  Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa
mada mama
Madam Sophy akimlisha keki mama yake mzazi wakati wa tukio hilo..
madamea
Mama Mzazi wa Sophy akimkumbatia mwanae
madama temy
Mwanadada, Hoyce Temu aliyejitoa kusaidia watanzania kupitia kipindi maalum cha 'MIMI NA TANZANIA' akilishwa keki na Madam Sophy katika tukio hilo
madamu temu
Hoyce Temu akimpongeza Madam Sophy kwa kuanzisha taasisi hiyo pamoja na kuandaa shughuli hiyo
mamdae
Madam Sophy akitoa nasaha zake juu ya hatua aliyofikia hadi kuanzisha taasisi hiyo.
mads
Baadhi ya watoto waliofika katika tukio hilo wakifanya maombi maalum kuwaombea wenzao wenye mahitaji maalum.
madac
baadhi ya watoto hao wenye ulemavu wa viungo
madam3
Madam Sophy akitoa nasaha zake
madaddd
Madam Sophy akikabidhi baadhi ya zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Makumbusho ambayo anafundisha pamoja na watoto wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu. Kwa picha zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages