Pages

KUMEKUCHA TAMASHA LA DINI LA UPENDO MUSIC FESTIVAL JUMAPILI YA PASAKA WASHIRIKI WAPO HAPA

Ikiwa zimebaki siku mbili yaani Jumapili ya Machi 27.2016 wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wanatarajia kushuhudia tamasha la dini la Upendo Music Festival ambalo litaambatana na matukio mbalimbali ndani ya viwanja vya Leaders Club.

Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited tayari imeweka wazi baadhi ya vikundi na wasanii washiriki wa tamasha hilo.
Baadhi ya Wasanii hao wenye kalama na upeo mkubwa katika kumuimbia Mungu wanaotamba ndani na nje ya Tanzania ni pamoja na: Angel Bernard, Emanuel Mbasha, Lynga George, Upendo Kihaile, Sarah Shilla, Faraja Ntaboba.

Pia wapo: Edson Mwasabwite, Angel Magoti, Abeid Ngosso, Ambwene Mwasongwe na Fridah Felix.

Aidha, washiriki wengine katika orodha hiyo ni pamoja na: Choir ya Kigogo KKKT, Gift and Beauty, Moses Saxer, Mise Ricprdias, The Joshua Generation, Glorious Worship Team, The Voice, Uinjilist Choir Kimara.
Wengine ni Doxers Praise Team, Calvary Band, The Jordan, The Next level, Chang’ombe Vijana Choir, Uinjilist Kijitonyaama, Tumaini Shangilieni Choir na wengine wengi.

Katika tamasha hilo hiyo siku ya Jumapili ya PASAKA, katika viwanja vya LEADERS CLUB, Kinondoni, linatarajia kuanza majira ya asubuhi ya nne ( 4:00) Hadi Saa 10:00 Usiku. Pia litajumuisha na Bonanza la Michezo, Michezo ya Watoto na Uuzaji wa Biashara mbali mbali
Kiingilio kawaida ni Tsh.5,000 na kwa viti maalum ni Tsh.10,000 huku kwa Watoto ni Tsh. 2,000.
“Music 100% Live, Njoo tumuimbie Mungu”.. Ulinzi na Usalama ni wa hali ya juu nyoote munakaribiswa.
abeddy_2
Abeid Ngosso
frida1
Fridah Felix
U36-620x399
Emanuel Mbasha Sarah Shilla
Sarah Shilla.
nightofhope17
Ambwene Mwasongwe.
Edson Mwasabwite
Edson Mwasabwite.
FB_IMG_1450057063985
Angel Bernard.
UPENDO MUSIC FESTIVALThe VoiceKundi la The Voice

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)