Pages

Kipindi cha redio cha Shuga charudi kwa kishindo

Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS   Abubakari Magege  akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
Mwakilishi wa UNICEF   Alice Ijumba  akijibu maswali ya washiriki wa
wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
 washiriki wa kipindi cha redio cha shuga wakifuatilia mada kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
Alice Ijumba toka UNICEF
Waratibu wa Shuga Radio drama series msimu wa pili - Pendo Laizer na David Sevuri wakichanganua ushiriki wa watangazaji na vikundi vya wasikilizaji
Mshiriki akichangia mada katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini;
Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa - TACAIDS,Fadhila Mturi  akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina elekezi





Vipindi vya redio vya Shuga vitaanza kuunguruma tena kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo vinalenga kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya kondomu na kuepukana na msongo rika.

Mfulilizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio yao,  changamoto wanazopitia ili kutimiza malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha yao ya kila siku.

Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga.

Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na mahudhui ya vipindi, mashirika ya UNICEF pamoja na TACAIDS kwa kushirikiana na kampuni ya True Vision Production wanaendesha mafunzo elekezi kwa vituo vya radio za jamii, mameneja wa radio shiriki, watangazaji na waandishi wa habari pamoja na kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za Halmashauri na Mkoa, ambapo warsha hii inafanyika mkoani Iringa.

Radio zitakazoshiriki katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni Clouds FM, Nuru FM – Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja na Furaha FM, Hope FM, Qibla Ten FM za Iringa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)