Pages

Bad News: DC Njombe, Sarah Dumba afariki dunia usiku

Akizungumza na Eatv, mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi amethibitisha kutokea kwa msiba huo, na kueleza kuwa marehemu Sarah amefariki majira ya saa moja jioni katika hospitali ya Kibena mjini Njombe ambapo alipelekwa kwa ajili ya uangalizi wa kiafya.
Dkt Nchimbi amesema kuwa, haijafahamika nini kilichosababisha kifo hicho, lakini huenda ikawa ni "Mshituko" maana leo asubuhi aliwasili ofisini kama kawaida, na kuendelea na shughuli zake akiwa hana tatizo.
Ameendelea kueleza kuwa, akiwa ofisini kwake, alianza kusema kuwa anajisikia vibaya, na kuamua kugawa majukumu yake kwa watendaji wengine, lakini hali yake ilizidi kutia mashaka na ndipo akapelekwa hospitali.
Dkt Nchimbi amesema, akiwa hospitali hali ilibadilika ndani ya muda mfupi na kuanza kutapika, na ilipofika majira ya saa moja alifariki dunia.
"Nadhani inaweza kuwa ni tension maana tupo kwenye maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji, na yeye amekuwa akishughulika sana na maandalizi hayo ambayo kilele chake ni kesho, sasa leo amefika ofisini kama kawaida, lakini baadaye akasema hajisikii vizuri, baadhi ya kazi akatuma watu, baadaye alikwenda hospitali, lakini muda mfupi baada ya kufika hali ikabadilika, akatapika sana na hapo ndipo alipopoteza maisha" Amesema Dkt Nchimbi.
Mkuu huyo wa mkoa amesema mipango ya maziko itatangazwa baadaye kesho, lakini kwa taarifa za awali alizonazo ni kwamba huenda akapelekwa nyumbani kwao ambapo ni Dar es salaam, ingawa kuna taarifa nyingine zi adai kuwa nyumbank kwao ni Morogoro.
Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu Sarah Dumba. Amin. Source EATV

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)