Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii.
KAMPUNI ya Jamii Media, waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com wametinga Mahakamani kufungua kesi ya kikatiba wakipinga baadhi ya vifungu vya sheria ya makosa ya mtandao kwa kile kuingilia Uhuru wa Maoni na Kujieleza wa wananchi.
Jamii Media imefungua kesi hiyo Mahakama Kuu leo jijini Dar es Salaam, kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa mahakamani, alisema kampuni hiyo imelazimika kufungua kesi hiyo baada ya kushinikizwa mara kadhaa na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za baadhi ya wateja wao.
Alisema takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huo kwa njia ya barua kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi.
Aliongeza kuwa JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri (privacy) wa wateja wao, wamekuwa wakihoji mashinikizo hayo yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja lakini wamekuwa hawapewi maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama hautatolewa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
"...Baada ya kupata mashinikizo takribani manne yanayoashiria kuwa haki ya watanzania watumiao mtandao wa intaneti na hasa watumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Jamii Media imeshauriana na Wanasheria wake na kuona ni wakati sasa wa Kuilinda haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa Uhuru wao wa Maoni na Kujieleza inayolindwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ibaraya 18 ambapo imefungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano," alisema Melo.
Alibahinisha kuwa mtandao wa JamiiForums utaendelea na shughuli zake kama kawaida na utaendelea kuwahakikishia watumiaji wake kuwa mahala salama pa kutolea madukuduku yao na hata kuisaidia Serikali kuonyesha nyufa zilipo kwa maslahi mapana ya Taifa (wakizingatia mwongozo wa ushiriki wa mijadala anuai).
Alisema JamiiForums itaendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi kwa kutoa uwanja/fursa salama na rahisi kwa wananchi kuweza kuyaainisha yale wanayoyabaini kuwa yanachelewesha maendeleo ya Taifa lao.
Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na Duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 4 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe. Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wana JamiiForums. "Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamotonyingi zinazopelekea waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara." Anasema Melo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)