WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF,JUMANNE MAGHEMBE AKUTANA NA WADAU WA UTALII MKOA WA KILIMANJARO. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF,JUMANNE MAGHEMBE AKUTANA NA WADAU WA UTALII MKOA WA KILIMANJARO.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa Utalii mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Baadhi ya Wadau wa Utalii wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii (hayupo pichani) alipokutana nao.
Waziri Maghembe akiwaeleza wamiliki wa kampuni zinazofanya shughuli za Utalii katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambapo aliwaeleza mambo mbali mbali yanayochangia kushusha pato la taifa .Miongoni mwa mambo aliyozungumza ni pamoja na kampuni za Utalii kutumia njia za Panya kupndisha wageni,Wapagazi kufa Mlima Kilimanjaro kutokana na baridi kali kwa kukosa mavazi maalumu ya baridi,Uchafu Mlima Kilimanjaro,Wageni kupatiwa huduma duni ,na mapunjo ya mishahara kwa wapagazi.
Mhifadhi Mkuu mpya wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akiwa katika kikao hicho ambapo alitamburishwa rasmi akichukua nafasi ya Erastus Lufunguro aliyehamishiwa Makao Makuu, Mhifadhi Loibooki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA).
Baadhi ya wamiliki wa kampuni za Utalii wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala akizungumza wakati wa kikao hicho.
Aliyekuwa Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, (KINAPA) Eva Mallya ambaye kwa sasa amehamishiwa Hifadhi ya Taifa ya Manyara akiteta jambo na Mhifadhi mkuu mpya wa KINAPA,Betrita Loibooki.
Katibu wa Chama cha Waongoza Watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko akiwasilisha malalamiko ya wapagazi mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii .(hayupo pichani)
Waziri Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi wakimsikiliza kwa makini katibu wa Chama cha Waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko (hayupo pichani ) alipokuwa akieleza changamoto.
Mkurugenzi Mkuu Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Utalii na Wadauu wa Utalii kilichofanyika mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa KGA,James Mong'ateko akikabidhi kwa Waziri Maghembe taarifa iliyohusu Changamoto mbalimbali wanazopata katika shughuli za kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Wadau wa Utalii katika kikao hicho. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii  Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages