Vitus akiwa ofisini kwake
Vitus akiwa nje ya jengo la kiwanda cha TBL cha Moshi
Vitus akiangalia Shahiri moja ya malighafi inayotumika kutengenezea bia
Asema mafanikio yoyote
yanatokana na kufanya kazi kwa bidii
Ukifika katika kiwanda cha TBL cha Moshi ambacho
kinatengeneza malighafi za kutengenezea bia kwa ajili ya viwanda vya bia
vilivyopo chini ya kampuni ya TBL na kukutana na Vitus Mhusi huwezi kujua kuwa
ni Meneja Mkuu wa kiwanda kutokana na muda wote anavyokuwa anachapa kazi na kusimamia shughuli za uzalishaji kwa
karibu kuhakikisha zinaenda vizuri.
Kwa kuzingatia misingi
ya uongozi bora Vitus muda wote huwa na ukaribu na wafanyakazi wenzake
na lijitokezapo tatizo la kikazi kama vile mitamo kuwa na hitilafu huakikisha
analivalia njuga kwa kushirikiana na wafanyakazi waliopo chini yake kulitatua
nafasi aliyonayo sio ya kubahatisha bali
anao ujuzi na uzoefu wa muda mrefu akiwa amefanya kazi katika viwanda vya bia
vya TBL nchini kwa zaidi ya miaka 35.
Katika mahojiano hivi karibuni Vitus alieleza kuwa akiwa
msomi wa fani ya sayansi upande wa kemia ametumia elimu yake katika maisha yake
yote kufanya kazi inayohusiana na
uzalishaji wa bia .
“Najivunia na kazi yangu na naipenda kwa kuwa utaalamu wangu
unachangia kuzalisha vinywaji vya bia bora ambazo zinatumiwa na watu wengi
sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi”.Alisema na kuongeza kuwa awaonapo
wanywaji wakiburudika na kinywaji cha bia husikia furaha sana na hasa ikizingatiwa
kuwa wapo watumiaji wengi ambao wanatumia kinywaji cha bia bila kujua kuwa
wataalamu wa kukitengenezwa wanatokea kwenye jamii wanazoishi na ni watu wa
kawaida.
Akielezea historia ya maisha yake Vitus ambaye katika maisha
yake yote amefanya kazi katika kampuni ya TBL anasema kuwa ni msomi mwenye
shahada ya Sayansi ya Kemia na Takwimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Mwaka 1987.
Alisema baada ya kuhitimu aliajiriwa na kampuni ya TBL kama
mtaalamu wa maabara kazi ambayo aliendelea nayo hadi alipofanikiwa kupata
nafasi ya kuongeza ujuzi katika fani ya kutengeneza bia katika Chuo Kikuu cha
Heriot Watt nchini Scotland kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya mwaka 1992 hadi
mwaka 1993.
Kabla ya kushika wadhifa alionao hivi sasa amepitia ngazi
mbalimbali za uongozi wa vitengo kwenye viwanda vya TBL “.Nimeongoza vitengo
mbalimbali katika kampuni ya TBL na nimejifunza mambo mengi yanayohusiana na
misingi ya utawala bora na uzalishaji wenye viwango”.Alisema.
Aliongeza kuwa kufanya kazi kwake sehemu mmoja katika maisha
yake kumemuwezesha kuielewa vizuri sekta ya uzalishaji bia kwa undani pia
ameweza kuhudhuria kozi nyingi za ndani zinazotolewa kwa wafanyakazi na aliifananisha TBL Group na Chuo cha mafunzo kutokana na kuwa na
mafunzo ya aina mbalimbali na ya kila mara kwa wafanyakazi wake ambayo
yanawasaidia wakiwa kazini na nje ya kazi.
Kuhusiana na mafanikio aliyoyapata kwa kufanya kazi
katika kampuni ya bia, alisema ni mengi
ikizingatiwa kuwa anafanya kazi kwenye kampuni kubwa inayojali maslahi ya
wafanyakazi wake “Mafanikio ni mengi ndio maana sijahama kwenda sehemu nyingine
tangu nianze kazi zaidi ya miaka 35 iliyopita,kutokana na kazi hii naweza
kuihudumia vizuri familia yangu”.Alisema.
Maoni yake kuhusiana na kukua kwa sekta ya uzalishaji vinywaji
nchini alisema hivi sasa imekua tofauti
na miaka ya nyuma ambapo hapakuwepo na ushindani katika sekta hii kama hali
ilivyo kwa sasa.
Kuhusiana na changamoto anazokutana nazo kwenye kazi yake
alisema kuwa ni za kawaida kwa kuwa hakuna kazi yoyote ambayo haina changamoto
kinachotakiwa ni kukabiliana nazo na kusonga mbele.
Mbali na kazi za kiwanda Vitus alisema kuwa ni mpezi wa
michezo mbalimbali hasa mchezo wa soka ambapo miaka ya nyuma alipokuwa kijana
alikuwa mchezaji wa kutumainiwa wa timu ya soka ya Pilsner iliyokuwa chini ya
kampuni ya TBL ambapo hivi sasa baada ya kuacha kucheza soka amekuwa akishiriki
katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon ambayo yamekuwa yakiandaliwa na
kampuni anayofanyia kazi ya TBL Group na kufanyika mkoan Kilimanjaro kila mwaka
na kuwavutia washiriki kutoka nchi mbalimbali.
Kuhusu maisha yake ya baadaye baada ya kustaafu alisema kuwa
atajihusisha na shughuli za kilimo na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na
fani yake.
Alimalizia wa kutoa wito kwa vijana waliopo mashuleni kusoma
kwa bidi li kupata taaluma zitakazowawezesha kufanya kazi kitaalamu na kuleta mabadiliko a kwa vijana waaoairiwa
kufanya kazi kwa bidii na kuwa na kiu ya kujiendeleza bila kusahau uwa
wavumilivu na waaminifu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)