TAMASHA LA CHANGIA DAMU KUFANYIKA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAMASHA LA CHANGIA DAMU KUFANYIKA LEO

Changia-damu-new
Tamasha la Changia Damu Okoa Maisha linatarajiwa kuanza leo katika Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam ambapo pia kutakuwa na wasanii mbalimbali.
Akizungumza na gazeti hili, Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligeisha alisema kuwa tamasha hilo litadumu kwa siku mbili kuanzia leo na kesho na kwamba watu wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
YAMOTO-BAND-2
Vijana wa Yamoto Band wanaoongozwa na Dogo Aslay.
“Lengo la tamasha hili la Changia Damu Okoa Maisha ni kukusanya lita kati ya 5,000 na 6,000 ambazo ni asilimia 75 ya mahitaji ya damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” alisema Eligeisha.

Eligeisha aliongeza kuwa tamasha hilo kama linavyojieleza, kwamba wachangiaji wa damu watakuwa wanafanya hivyo ili damu hiyo ipelekwe benki ya damu kwa ajili ya wagonjwa watakaoihitaji.

“Pia kutakuwepo na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza bure wakiwemo vijana wa Yamoto Band wanaoongozwa na Dogo Aslay pamoja na wasanii kutoka nyumba ya kuibua vipaji ‘ THT’ ambao watafanya vitu vyao wakati zoezi hilo likiendelea,” alisema.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, Clouds FM, Pepsi Tanzania, Startimes, Abbott Fund, Benki ya CRDB, Mfuko wa Pensheni wa GPEF pamoja na Motisun Group Tanzania Ltd.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages