NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH.ASHATU KIJAJU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKAA WA 25 WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH.ASHATU KIJAJU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKAA WA 25 WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF

833A7768
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
833A7530
833A7535
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko"unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
833A7594
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju.
833A7795
 Baadhi ya Wadau washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju alipokuwa akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
833A7847
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
833A7882
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
833A7615
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
833A7663
Mmoja wa wanachama wa Mfuko wa PPF mwenye ulemavu wa kusikia akiendelea kufatilia mada mbali mbali kwenye mkutano huo kupitia mkalimani wa lugha ya alama.
833A7666
Wadau wakipitia kablasha la PPF.
833A7736
833A7972
833A7977
833A7996
833A8021
833A8029
833A8057
833A8073
833A8089
833A8150
833A8207
833A8219
833A8262
Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF.
833A8276
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akitoa hotuba fypi ya shukrani kwa niaba ya mifuko ya hifadhi za jamii nchini.
833A7512
833A7608
833A7553

833A7558
833A7571
833A7637
OTH_8915

OTH_8924
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
833A8307

833A8314

833A8376

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages