Rais wa Tanzania
John Magufuli amesema amesikitishwa sana kitendo cha kuuawa kwa rubani
Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na
ujangili.
ana na majangili
katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.
Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa kisa hicho.
Tembo watatu pia walipatikana wakiwa wameuawa.
Dkt
Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua
rubani huyo wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria,
kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu.
Polisi tayari wamewakamata
washukiwa watatu kuhusiana na mauaji hayo.
Kiongozi huyo amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote.
Amewataka
wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa
tamaa na tukio hilo na wasaidie kuwafichua watu wote wanaojihusisha na
ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.
Hivi
karibuni, utawala nchini Tanzania umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa
kutoa maelezo ya kina kuhusiana na uwindaji haramu wa pembe za ndovu.
Uwindaji
haramu umeenea sana katika pori ya Maswa na sio tukio la kwanza ambapo
wanaharakati wanaolinda wanyama wa porini wanashambuliwa na wawindaji
haramu.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)