flydubai yatangaza mwaka wake kamili wa nne wa faida na ongezeko la 25% katika idadi ya wasafiri
Kampuni hii ya ndege inaendeleza hadithi ya ukuaji
· Inatangaza Matokeo ya Kila Mwaka ya 2015 na kuripoti faida ya AED milioni 100.7 (USD milioni 27.4)
· Jumla ya mapato ilikuwa AED bilioni 4.9 (USD bilioni 1.33) kwa kipindi cha miezi 12
· Kampuni hii ya ndege iliwabeba abiria milioni 9.04 kwenye mitandao yote. Ongezeko la abiria milioni 1.8 lilikuwepo ikilinganishwa na wale wa mnamo mwaka wa 2014; ongezeko zuri la 25%
· Jumla ya safari 81,530 za ndege mwaka mzima
· Urefu wa sekta ya wastani ulikuwa 1,664 km kwenye nusukipenyo ya eneo hilo la kijiografia
Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Februari 10 2016: leo flydubai iliripoti faida ya AED 100.7 (USD milioni 27.4 ) ya mwaka 2015 baada ya nusu ya pili ya mwaka yenye nguvu zaidi ambayo ilishuhudia ongezeko kwenye idadi ya abiria waliosafiri kwenye mtandao wake wote.
Jumla ya mapato ya mwaka mzima ilikuwa AED bilioni 4.9 (USD bilioni 1.33), ongezeko la 11% likilinganisha na mwaka wa 2014. Mapato ya jumla, kulingana na hesabu za Mapato kwa kila Abiria na Kilomita (RPKM), yalikuwa na ushindani mkubwa kutokana na dola yenye nguvu; mazingira ya kufanyia kazi kwenye mitandao yote yenye changamoto; kutatizwa kwa usafiri kutokana na kusitishwa kwa safari za ndege kwenye baadhi ya njia maarufu na idadi kubwa ya njia zilizozinduliwa hivi majuzi huku muda wa kuongoza ukihitajika ili kuweza kufikia ukomavu.
Muadhama Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, Mwenyekiti wa flydubai, alisema: “2015 ulikuwa ni mwaka muhimu kwa flydubai. Ulikuwa ndio mwaka ambao kupitia kwa bidii na kujitolea kwetu tuliendelea kufikia dira yetu ya kuongeza mwunganisho katika kusaidia maendeleo ya kiuchumi ya UAE. Mwaka uliisha huku nasi tukisherehekea mafanikio mawili: kuletwa kwa ndege yetu ya 50 na mwaka wetu wa nne wa faida.”
Ghaith Al Ghaith, Ofisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa flydubai, aliongezea na kusema: “Mazingira ya jumla ya kufanya biashara yameendelea kuwa changamoto lakini tumeendeleza hadithi yetu ya ukuaji nao mwaka umeisha vizuri. Ukuaji wetu wa abiria wa 30%, kulingana na RPKM, unatilia mkazo utashi wa usafiri ndani ya zingatio letu la kijiografia; kivutio kisichoisha cha Dubai kuwa hatma ya usafiri; na umaarufu wa huduma yetu.”
Matokeo ya gharama
Matokeo bora zaidi kwenye nusu ya pili ya mwaka pamoja na jitihada za usimamizi wa gharama yamesababisha mwisho mzuri wa mwaka huu.
Gharama za mafuta zilipungua kwa 30.3% ya gharama za utendakazi zikifaidi kutokana na bei za chini za mafuta huku 59% ya gharama za mafuta zikiwa hazina mipaka. Kulingana na sera ya kuweka mafuta ya flydubai, mahitaji ya mafuta ya 16% kwa miezi 24 kwa sasa yamewekewa mipaka. Hali hii itaweza kuhakikisha kwamba kuna kiwango cha uhakika na udhibiti wa gharama zake za mafuta kutokana na kuyumbayumba kwa bei za mafuta.
EBITDAR ilipungua kidogo ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, laikini ilibakia katika hali nzuri kwa 20.5% ya mapato.
Kiwango cha hela cha kufunga mwaka na visawe vya hela husika, yakiwemo malipo ya kabla ya uwasilishaji wa ndege kwa zile ndege za kuwasilishwa siku za usoni, zilikuwa nyingi kufikia AED bilioni 2.4.
Ghaith Al Ghaith, Ofisa Mkuu Mtendaji wa flydubai, akizungumzia kuhusu gharama ya utendakazi wa flydubai, alisema: “Msingi thabiti tuliouweka wakati ambapo kampuni hii ya ndege ilipozinduliwa umehakikisha kwamba tuko katika hali bora zaidi ya kuitikia kwa haraka katika kukabiliana vikali na changamoto kwenye mazingira ya kijamii na kiuchumi, kwa njia ya kudhibiti, kwa muda wa kipindi kifupi na hata kipindi kirefu.”
Matokeo ya utendakazi
Tayari kwa biashara: Daraja la Biashara lilianzishwa kwenye njia mpya 17 mnamo 2015 zikiwakilisha 87% ya safari zote za kutoka Dubai. flydubai iliweza kushuhudia idadi ya abiria kutoka kotekote kwenye mtandao wake ambao walisafiri daraja la biashara likiongezeka kwa 72% tukilinganisha na mwaka wa 2014. Utashi wa juu zaidi ulitokea Afrika ukifuatwa na Mabara yale madogo na hata Mashariki ya Kati, ikiangazia utashi wa usafiri wa daraja la biashara hewani, hususan kwenye masoko ambayo hayajawa na ufikivu wa huduma hii hapo awali. Utashi wa huduma hii unaonyeshwa pia katika mkao wa UAE kikiwa kituo cha kimataifa kinachotambulika kibiashara na ununuzi.
Kuendesha utashi katika kitovu cha pili: kuanza kwa operesheni mpya za flydubai katika sehemu ya Al Maktoum International-Dubai World Central kuliweza kushuhudia huduma hizi zikipatikana kwa sehemu nyingine kama vile Amman, Beirut, Doha, Kathmandu na Kuwait huku safari za ndege za kuelekea kwenye sehemu hizi zikiendelea kupatikana katika Dubai International. Huduma hizi zilianza tarehe 25 Oktoba 2015 na katika wiki hizi za kwanza 10 za operesheni abiria walikaribisha chaguo hili na utulivu huu uliotolewa kwenye angatua hii mpya. Al Maktoum International-Dubai World Central ni sehemu inayoendelea kutoa abiria kutoka kotekote Dubai huku kukiwa na fursa zlizoongezeka za usafiri.
Kuunda usafiri wa kufanya biashara bila malipo: ufikivu ulioongezeka katika masoko ambayo yalikuwa hayajashughulikwa hapo awali umefaidi mapato ya ubebaji mizigo ambayo yanabakia kuwa thabiti, yakionyesha ongezeko la 28.4% huku mizigo ipatayo tani 40,441 kwenye mwaka huu.
Ongezeko la mapato ya ziada kutokana na kugharimika kwa abiria: utendakazi thabiti ulioendelea kwa mauzo kabla na ndani ya ndege yakiwemo yale ya burudani ya ndani ya ndege, chakula, mapendeleo ya kiti, marupurupu ya mzigo wa ziada, kukodisha gari, bima ya usafiri na huduma za uratibu wa visa zilichangia mapato yapatayo 15.1%. Uanzishwaji wa teknolojia mpya umeweza kusababisha wepesi na fursa zaidi za ongezeko la mauzo.
Kukua kwa uzoefu na kwa vipaji: katika kuunga mkono idadi zake za ndege idadi ya wafanyikazi wa flydubai iliongezeka hadi kufikia kiwango cha 3,393 wakiwemo rubani 658, watoaji huduma ndani ya ndege wapatao 1,435 na wahandisi 273 wote wakiwakilisha mataifa 114. Hali hii inaonyesha fursa iliyoundwa kwa kufungua masoko ambayo hapo awali yalikuwa hayajashughulikiwa na uwezo wa flydubai katika kuvutia baadhi ya vipaji bora zaidi katika kiwanda cha masuala ya ndege.
Kusikiliza wateja wetu: uchunguzi wa ndani ya ndege wa flydubai unaendelea kupatia kampuni hii ya ndege maono ya kipekee katika kushughuilikia mitindo ya usafiri inayoibuka. Maoni kupitia kwenye uchunguzi wa ndani ya ndege yalitolewa na abiria 230,016 na yaliweza kugusia sehemu za usafiri zipatazo 36. flydubai inahakiki na kuchanganua data kila wiki na kuitumia kuendesha ugunduzi kotekote kwenye kampuni hii ya ndege. Mtazamo huu unatilia mkazo zaidi kujitolea kwa kuweka hali anayopitia mteja katika hali ya kipaumbele katika operesheni zake.
Kuunda muunganisho halisi: mikakati ya flydubai ya kuunga mkono lengo la Serikali na kuunda kituo cha biashara na utalii katika kilichotambulika kote ulimwenguni imeweza kushuhudia:
· flydubai ikizindua sehemu 18 mpya za usafiri zikiwemo Asmara, Astana, Chennai, Gizan, Jouf, Quetta na Shiraz.
· Ongezeko katika biashara na usafiri wa starehe kati ya KSA na UAE lilichangia katika soko la flydubai kwa 26%. Kujitolea kwa flydubai katika kufungua viungo vya usafiri wa hewani wa moja kwa moja kati ya angatua za kimaeneo za KSA's na Dubai kuliweza kushuhudiwa idadi ya safari za ndege ikongezeka kwa 29% ukiwemo mwanzo wa safari za kwanza za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jouf.
· mtandao jumlishi wa flydubai kotekote GCC (ikiwemo Bahrain, Kuwait, Qatar na Oman) uliweza kushuhudia idadi ya abiria ikikukua kwa 18%.
· Idadi ya abiria kutoka alama 14 za Mashariki ya Kati (zikiwemo sehemu za Jordan na Lebanon) ziliongezeka kwa 37%.
· Utashi wa usafiri kati ya India na UAE uliendelea kuwa thabiti. flydubai iliweza kuandikisha 15% ya jumla ya abiria waliongezeka ambao waliwakilisha 4.5% ya jumla ya soko. Mnamo Machi, Chennai ilikuwa ndio sehemu ya 8 katika mtandao wa flydubai nchini India kuwa na safari za ndege tatu kwa wiki.
· Huku sehemu 11 kule na sehemu 9 kule Urusi idadi ya abiria wa flydubai ilikuwa kwa 14% kotekote kwenye masoko haya hata hivyo idadi ya abiria ya Urusi na Dubai ilipungua kwa 22% ikionyesha hali ya sasa ya kiuchumi.
· Idadi ya abiria kutoka Caucasus iliongezeka kwa 21% na kutoka Esia ya Kati kwa 15%.
· Kuanza kwa safari za ndege kuelekea Quetta na Faisalabad kulishuhudia mtandao wa sawa Pakistan ukiongezeka katika sehemu tano na ongezeko la 77% kwa idadi ya abiria pia likachangia katika ukuaji wa jumla wa soko hilo kwa 12%.
Tangu kuzinduliwa kwake, flydubai imefungua sehemu za kusafiria 59 kwenye mtandao wake ambazo awali zilikuwa hazihudumiwi au ambazo hazikuwa na kiungo cha usafiri wa hewa cha moja kwa moja hadi Dubai. 2015 iliweza kushuhudia flydubai ikiongeza muunganisho wake uliotolewa na kitovu cha masuala ya ndege cha Dubai na kuchangia 29% ya ongezeko la abiria waliokuwa wakitumia angatua za Dubai.
Kuzidisha ndege za kisasa na zenye ubora: flydubai iliweza kugharimika na kuleta ndege saba mpya kwenye mwaka wa 2015 ambazo zilijumuisha ndege yake ya 50 huku ikiadhimisha kuletwa kwa ndege ya mwisho kutoka kwenye agizio la kwanza la ndege lililotolewa katika Maonyesho ya ndege ya Farnborough mnamo mwaka wa 2008. Matumizi ya ndege yalikuwa saa nzima 13.6 pamoja na rekodi inayoongoza kwenye kiwanda cha ndege ya 99.77% ya kutegemea utekelezaji wa kiufundi wa ndege hizo.
Ghaith Al Ghaith, Ofisa Mkuu Mtendaji wa flydubai, akizungumzia kuhusu operesheni za utendakazi wa flydubai, alisema: “Tumekuwa tukizingatia kuzidisha ufikivu wa Dubai na kwenye miaka miwili iliyopita tumeweza kuzindua njia mpya 41. Katika kuunga mkono mipango yetu ya upanuzi, tumeendelea kuunda utashi wa usafiri huku tukiendeleza ubora wa operesheni zetu na kutimiza mahitaji ya abiria wetu.”
Muonekano
Kuanzia Mei, flydubai itaweza kupokea ndege mpya 16 ndani ya miezi 24 ijayo. Ndege hizi zinajumuisha ndege kubwa mpya aina ya Boeing 737 MAX 8 ambayo inatarajiwa kuwasili kwenye nusu ya pili ya mwaka wa 2017. Katika kwenda sambamba na mikakati yake ya kuendelea kuwa na ndege changa na bora ndege hizi zitaweza kusaidia ukuaji unaoendelea wa flydubai pamoja na kusawazisha baadhi ya zile ndege asilia kwenye kundi hili. Katika kipindi hiki, ndege saba zitaacha kutumiwa.
Kuendelea kuzingatia upunguzaji wa gharama na jitihahada za kuboresha ubora wa operesheni ni vitu vinavyotarajiwa kuchangia katika kupunguza gharama zaidi za kampuni hii ya ndege.
Mtandao wa njia ya kampuni hii ya ndege utaendelea kupata nguvu unaposhuhudia njia hizi zote mpya 41 zikizinduliwa kwenye miaka kamilifu miwili iliyopita. flydubai ina mtandao wa sehemu za kusafiria 89 katika nchi 43.
Ghaith Al Ghaith, Ofisa Mkuu Mtendaji wa flydubai akizungumzia kuhusu mwaka ujao, alisema: “Mtandao wetu unakomaa na hivyo basi tunaendelea kufuatilia uwezo na kuhakiki fursa ya njia zilizopo pamoja na njia mpya. Katika kuitikia mazingira yanayobadilika, yanatiliwa maanani, marekebisho yenye usawazisho na usimamizi ni vitu ambavyo vitahitajika. Mtazamo wetu wa bidii utasaidia flydubai kubakia katika hali-nzuri ya kutumia nafasi hiyo nzuri ya fursa zilizo ndani ya eneo letu la kupaa hewani na kuendelea na ukuaji wa safari zetu kwa njia endelevu.”
-Mwisho-
Multimedia content
- Download logo
- Image: CEO of flydubai, Ghaith Al Ghaith
- Image: flydubai Business Class Cabin
- Image: flydubai aircraft
- Image: flydubai Boeing 737-800 NG Aircraft
- Document: flydubai Route Map (February 2016)
- Document: خارطة وجهات فلاي دبي
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:
Houda Al Kaissi, Mtaalamu wa Mahusiano ya Umma, flydubai (+971) 56 683 0336; Baruapepe:houda.alkaissi@flydubai.com
Kareem Mahjoub, Ofisa wa Wanahabari, flydubai: (+971) 55 635 6196; Baruapepe: kareem.mahjoub@flydubai.com
Kuhusu flydubai:
Flydubai iliyopo Dubai inalenga katika kuondoa vizuizi vya usafiri na kuzidisha muunganisho kati ya tamadauni tofauti kotekote kwenye mtandao wake unaozidi-kuongezeka. Tangu kuzinduliwa kwa opersheni zake mnamo 2009, flydubai imeweza:
· Kuunda mtandao wa sehemu za kusafiria 90, pamoja na njia mpya 18 zilizozinduliwa mnamo 2015.
· Imefungua njia mpya 59 ambazo awali hazikuwa na kiungo cha usafiri wa hewa wa moja kwa moja hadi Dubai au hazikuhudumiwa na ndege ya kitaifa ya UAE kutoka Dubai.
· Imejenga kundi la ndege mpya zipatazo 50 aina ya Next-Generation Boeing 737-800 na itapokea zaidi ya ndege aina ya 100 Boeing kufikia mwisho wa mwaka wa 2023.
Aidha, wepesi na urahisi na unyambukaji wa flydubai ikiwa ni kampuni ya ndege changa umezidisha maendeleo ya kiuchumi ya Dubai, kulingana na maono ya serikali ya Dubai kwa kuunda biashara na mtiririko wa watalii.
Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma za flydubai, tafadhali tembelea flydubai.com.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)